Michael Amon
JF-Expert Member
- Dec 22, 2008
- 8,768
- 3,622
Jinsi ya kupika pweza
Mahitaji
Jinsi ya kupika
Mahitaji
[*=left]70 gram kitunguu swaumu
[*=left]150 gram kitunguu maji kata kata
[*=left]150 gram karoti kata vipande vidogo
[*=left]1 pilipili ya kijani fresh a pili pili mbuzi
[*=left]1 kijiko kidogo cha chai unga wa korienda au girigilani
[*=left]200 gram viazi ulaya
[*=left]10 gram chumvi
[*=left]150 gram pilipili hoho
[*=left]160 ml mafuta ya kupikia
[*=left]70 ml juisi ya limao
[*=left]500 gram nyanya ya kopo
[*=left]350 ml Maji
[*=left]1 kilo ya pweza kata kata vipande vidogo vidogo
- Weka mafuta katika sufuria kisha acha ya pate moto.
- Baada ya hapo weka kitunguu maji kaanga kwa dakika 1 kisha weka kitunguu swaumu kaanga tena kwa dakika 1.
- Weka pweza na viazi ulaya kaanga kwa dakika 10 - 15 kwa moto wa wastani.
- Kisha weka unga wa korienda, caroti, pili pili hoho, chumvi, pili pili mbuzi, juisi ya limao kaanga kwa muda.
- Kisha weka nyanya ya kopo na koroga vizuri kisha weka maji acha ichemke kwa dakika 5 mchuzi upungue pweza wako atakua ameiva.