Nyambari Nyangwine: Umechangia Kuharibu Elimu ya TZ

kikilo

Senior Member
Joined
Jan 13, 2013
Posts
114
Reaction score
70
Nilikusikiliza jana unlipokuwa unachangia hotuba ya wizara ya mambo ya vijana michezo na utamaduni, huku ukiwaponda wanamziki wa kisasi kipya. Katika mchango wako kilichoniudhi ni kitendo cha kudai kuwa wewe ni mchapishaji wa vitabu mnastahili kusaidiwa na serikali kuliko wanamuziki wa kizazi kipya.

Ndugu yangu Nyambari wewe unapaswa kulaaniwa kwa uchafu uliouleta kwenye mfumo wetu wa elimu kwa kuchapisha vitini. Wewe ni mchafuzi wa elimu. Umechangia kulingamiza taifa, Unapaswa kuogopwa kama ukoma, maana umepenyeza rushwa mpaka vitini vimekuwa vitabu vy kiada shuleni.
 
The day, Monday 20 May 2013 need be highly commemorated by Nyangwine Nyambali Chacha Maliba for it is the day he DARED TO EXPOSE HIS POLITICAL NUDITY IN THE HOUSE..
 
Nashangaa eti vitabu vya mtu kama huyu vinatumika shuleni!Siwezi kushangaa kuona utaahira unaongezeka kwa wahitimu wetu iwapo vitabu ndo vya huyu jamaa!Mbona anaonekana kuwa na uwezo mdogo sana kiakili?

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Nashangaa eti vitabu vya mtu kama huyu vinatumika shuleni!Siwezi kushangaa kuona utaahira unaongezeka kwa wahitimu wetu iwapo vitabu ndo vya huyu jamaa!Mbona anaonekana kuwa na uwezo mdogo sana kiakili?

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
Ndio nchi yetu hii kila kitu kinawezekana hakuna consistence kwa utajiri wa mtu, unaweza amaka january 2013 huna kitu kabisa na umekata matumaini lakini kufikia December wewe ni millionaire kutokana na kukutana na deal za ajabu ajabu kama hizi za kina Nyambari Nyangwine
 

nakumbuka mwalim wetu wa history A-level alitupiga marufuku kutumia vitabu vya nyangwine maana ni vya hovyo sana
 
dah namkumbuka huyu jamaa nilikremisha kitabu kizima cha history notes na history questions and answers.
Ambavo havikuwa na tofauti kabisa
 
hapa sawa
Tatoo, VITA NI VITA. Si afadhali uneomba uwanja wa michezo wa mpira ili tupunguze vita ya mapanga Poti. Je unajua kuwa vitabu vyako vinachangia kuua elimu Tanzania?
Du ama kweli CCM ni nambari one kwa kuwa na wabunge wa aina yako.
TAFAKARI!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Yeye mwenyewe sio intellectual sasa vitabu anaandikaje, nasikia na cha Makamba kiitwacho Rushwa katika biblia na quran karibu kitatumika kwenye sylabus, ndio maana sishangai nikiona wanafunzi wanaandika MA-ZOMBIE HAYAJAVAA VIATU.

Kuna vitabu vyeney maana na mantiki vinatakiwa virudishwe kwenye sylabus mfano,wasifu wa siti binti, saad,kusadikika,kufikirika,Kisima cha Giningi,Lila na Fila ,kuli,bogonoka na Ntulanalwo,amkani si shari tena,shetani msalabani etc.

Hizi ni aina za vitabu ambavo uongeza uwezo wa mwanafunzi wa kufikiri na kuchambua mambo mbalimbali,kuliko vitabu vya siku hizi vya akina Nyangwale na summary zake ambazo uwafanya wanafunzi wasisome vitabu bali wananunua summary na kisha kwenda kwenye mitihani.
 
Mwache ajifurahishe nafsi yake maana hili ndilo bunge lake la kwanza na la mwisho katika maisha yake maana wana Tarime wanataka mabadiliko na sio legelege
 
Pole Mura waneh.

Tatizo ni kwamba unapoiga jambo fikiri kwanza. Usiwaige kina Muchamba Mwinguku, huyo an zake anazopewa. Hivi najiuliza, Je, Ni lazima uchangie kila hoja? Mura, ukikaa kimya itakugarimu nini? Mbona ulitoa harufu chafu hivyo kule mjengoni?

Ningepewa ruhusa na uma wa Tz vitabu vyako ningeamuru virudishwe vyote na ukavichome kwa garama yako. Mbona TFDA mnaonea hivi? Poda inachbua uso lakini haiharibu akili, Vitabu vya huyu Mura ndivyo vimeharibu elimu yetu atatokea wapi mtaalamu wa kupima vyakula baada yako wewe mchunguzi? TAFAKARI!

NYAMBARI NI SUMU YA MAMBA kwa lizazi chetu
 
Nashangaa eti vitabu vya mtu kama huyu vinatumika shuleni!Siwezi kushangaa kuona utaahira unaongezeka kwa wahitimu wetu iwapo vitabu ndo vya huyu jamaa!Mbona anaonekana kuwa na uwezo mdogo sana kiakili?

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums

halafu kwa ujasiri eti anajiita mchapishaji, nimeshawapiga marufuku wanafunzi wangu kuvitumia kama reference vitabu vyake huyu jamaa, kuna mwandishi wake wa kitabu cha physics kanikera sana error na uongo kibao hesabu hivohivo, huyu jamaa vitabu vyake vipigwe marufuku ni UCHAFU!
 
kama shule ulisoma zaidi vitabu vya nyangwine utajigundua u mtupu kihoja...jaribu kujichunguza..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…