DOKEZO Nyamongo Kuna Shida gani na Wawekezaji wa Mgodi wa North Mara Kiasi kwamba Vurugu Zinazokatisha Maisha ya Watu Hazikomi?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Huwa nashangaaa sana sana kumuona mtanzania maskini... Hata shati amevaa limetoboka.... Hata 100 hana lakini anasema "CCM oyeeeee...."
Anyway za kiafrica ni....
 
Wakurya wana matatizo sana! Ujuaji na matumizi ya nguvu ni mengi sana!

Wanasiasa pia wanatumia mgogoro huo wa mgodi na wakazi wa Nyamongo kujipatia umaarufu!

Wataendelea kufa kama serkali isipo acha siasa na kuchukua maamuzi ya kuwatoa na kuwalipa wananchi ili watoke maeneo hayo!
Haujui ulisemalo mkuu, vizuri kuto kuchangia kila uzi kama hauna uhakika na hoja yako
 
Labda tungejua mauaji yametokea lini, eneo gani na kwanini na nani aliyefanya mauaji
kwa tetesi zilizopo inasemekana kwamba......
Vijana wanao ingia kuiba mawe yenye dhahabu waliwavamia polisi na kuwajeruhi (mkono inasemekana ulivunjika na mwingine pua ili jeruhiwa vibaya) katika mgodi huo kule gokona eneo la ukipita mataa kama unaelekea uwanja wa ndege.
Baada ya hapo askari wale wanao fanya doria nje ya uzio wa mgodi walijibu mashambulizi na kupelekea chamoto kumdedisha intruder mmoja.
 
Haujui ulisemalo mkuu, vizuri kuto kuchangia kila uzi kama hauna uhakika na hoja yako
Kaka usijitie kujua sana! Hakuna mlinzi wa mgodi atapiga risasi mtu kama hujaenda maeneo ya mgodi! Mbona Kahama,Merelani au Geita hayatokei iweje Nyamongo?
Mfano Tegesha kwa kujenga nyumba kwenye maeneo ya mwekezaji pia baadhi ya vijana kuingia ndani ya mgodi kuchukua au kuiba mawe yanayosadikika kuwa na dhahabu nalo unakataa!?
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa ndo hayo Wakurya yanawakuta!
 
kwa tetesi zilizopo inasemekana kwamba......
Vijana wanao ingia kuiba mawe yenye dhahabu waliwavamia polisi na kuwajeruhi (mkono inasemekana ulivunjika na mwingine pua ili jeruhiwa vibaya) katika mgodi huo kule gokona eneo la ukipita mataa kama unaelekea uwanja wa ndege.
Baada ya hapo askari wale wanao fanya doria nje ya uzio wa mgodi walijibu mashambulizi na kupelekea chamoto kumdedisha intruder mmoja.
Kwa hapa nimekupata mkuu. Hv sasa taarifa hizi hazienei kama zamani. Lakini pia hii imesababishwa kwa kiasi kikubwa mgodi kusitisha kwa kiasi kikubwa ajirq za upendeleo kwa wakaazi/wazawa wenye sifa. Lakini vilevile kitengo cha Mahusiano ya jamii hivi sasa hakifanyi kazi jyake kwa ufasaha ambayo ni kuungajisha jamii na mgodi. Siku hizi wanaajiri maafisa mahusiano toka maeneo ya nje ambapo afisa mahusiano anakuwa hajui jiografia ya eneo, lugha na tabia za wazawa hivyo kutopata ile bond kama ilivyokuwa zamani.
 
Mlitaka waajiri Wakurya tu kisa kulinda mahusiano!
Siku hizi hata kijijini watu wanaongea Kiswahili! what kind of mahusiano you are talking about?
Kama vijana wa maeneo hayo hawana ujuzi mwekezaji lazima atafute watu wenye ujuzi kutoka maeneo tofauti,Kakola Bulyanhulu kuna kila jamii ya watu wa nchi hii wameajiriwa ,hata GGM na Mererani!
Unapotaka kupendelewa kwenye ajira huku huna taaluma inayokubeba badala yake uanaleta hasira na ujinga lazima upasuke no matter itakuwaje!
Somesheni vijana wawe na elimu ya ufundi na taaluma zinazoendana na mwekezaji wa maeneo hayo!
 
Serikali pamoja na watu wa Nyamongo njoo I hapa mtueleze shida ni ni ipi kati yenu na wawekezaji wa mgodi wa North Mara Kiasi kwamba vurugu Kila mara?

Vurugu hizi zimekuwa zinachukua maisha ya watu na zilianza miaka Ile ya Mkapa Hadi Leo hii Bado ni shida.

Na nyie Chadema ambao nmachukulia siasa na kuchochea watu walete vurugu mnanufaika vipi na hasara ya uhai wa watu?

Mbona migodi Iko Mingi sana hapa Tanzania lakini Kwa nini Kila mara ni huko Nyamongo tuu?

View: https://www.instagram.com/reel/C5lBKG0KZyx/?igsh=b3R6Z204NnE5MDVh

My Take
Serikali tumeni watu wa Elimu Kwa Umma na Kisaikolojia wakawasaidie hao watu lakini pia muwadhibiti Wanasiasa wanaoshadidia vurugu hasa Chadema.

Chadema imefanya fujo sana kule,watu wanauawa mnoo,mwaka ule wangwe alianzisha maandamano makubwa sana kwenda eti kudai madini yao mgodini,watu wakafa na kuumia,chadema ikaona huo ni mtaji kisiasa,hovyo sana.
 
Kaka usijitie kujua sana! Hakuna mlinzi wa mgodi atapiga risasi mtu kama hujaenda maeneo ya mgodi! Mbona Kahama,Merelani au Geita hayatokei iweje Nyamongo?
Mfano Tegesha kwa kujenga nyumba kwenye maeneo ya mwekezaji pia baadhi ya vijana kuingia ndani ya mgodi kuchukua au kuiba mawe yanayosadikika kuwa na dhahabu nalo unakataa!?
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa ndo hayo Wakurya yanawakuta!
Sio najifanya kujua chief...
Ukweli ni kwamba najua.
Ngoja nianze kwa kukufahamisha namna hii....
1. Migodi kama Bully, Buzwagi, Geita hawavuni kifusi madini chenye visible gold na hii ndio sababu ya inruders kuto kusumbua maeneo hayo kwa uvamizi.
Mgodi wa Tulawaka ulikua na visible gold na hii ilikua inapelekea hadi zaidi ya wangoni/intruders 1000 kuvamia RomPad (na ule ukanda wavamizi walikua wingi ni wanyantuzu na wasukuma.
Mgodi wa North Mara unakifusi madini chenye visible gold na hii ndio chanzo hasa cha wenyeji wa kule kuvamia kwasababu kazi kidogo pesa nyingi (hapa tunaongeza na ujeuri wao wa asili).
Kimsingi hakuna mlinzi wa mgodi anae ruhusiwa hata kumshambulia mvamizi na sheria inawataka wanapo waona wavamizi watoe taarifa kwa polisi ambao hufanya doria kwenye maeneo yoote ya mgodi nje na ndani ya uzio.
Kuhusu tegesha, yale ni mashamba ya wakazi ama wenyeji wa Nyamongo, Nyarero, Nyabichune, Kerende na kadhalika. Hivyo basi Barrick anapaswa kulipa fidia wenye mashamba/maeneo yao baada ya kufanya utafiti na kuona kama anapataka ili avune/achimbe dhahabu.
Mkuu hadi sasa maeneo yanayo julikaana North Mara anayamiliki rasmi ni Nyabirama na Gokona.
Upo nyonyo....🤔
 
Mlitaka waajiri Wakurya tu kisa kulinda mahusiano!
Siku hizi hata kijijini watu wanaongea Kiswahili! what kind of mahusiano you are talking about?
Kama vijana wa maeneo hayo hawana ujuzi mwekezaji lazima atafute watu wenye ujuzi kutoka maeneo tofauti,Kakola Bulyanhulu kuna kila jamii ya watu wa nchi hii wameajiriwa ,hata GGM na Mererani!
Unapotaka kupendelewa kwenye ajira huku huna taaluma inayokubeba badala yake uanaleta hasira na ujinga lazima upasuke no matter itakuwaje!
Somesheni vijana wawe na elimu ya ufundi na taaluma zinazoendana na mwekezaji wa maeneo hayo!
Kwa hili nakuunga mkono kamili.
Pale mwanzo wenyeji wa Nyamongo walikua hawasomeshi watoto kabisa wakitarajia watapigana na muwekezaji hadi aondoke..🤣 kumbe ikawa kinyume chake, mzungu akajaza polisi kwaanza kula kichapo hadi wakaanza kunyooka, then mgodi ukaanza kuchukua watoto wa wenyeji wa vijiji vinavyo zunguka na kupakana na mgodi wakawapeleka MTT Moshi kwaajili ya kupataa ujuzi, then kampuni hiyohiyo ikaanza kuwaajiri vijana hao na matokeo yake vijana wakaanza kua wezi na wadokozi katika mgodi, then muwekezaji akaamua kuacha kuwasomesha tena...😜
 
Sina maana hiyo mkuu. Sishadadii hizo ajira za kujuana lakini ziko sababu kwanini hao wananchi wanakuwa na tamaa ya kuvamia. Mikataba mingi iliyoahidiwa kunufaisha jamii ya wenyeji, hivi sasa imekaliwa na wanasiasa
 
Sio najifanya kujua chief...
Ukweli ni kwamba najua.
Ngoja nianze kwa kukufahamisha namna hii....
1. Migodi kama Bully, Buzwagi, Geita hawavuni kifusi madini chenye visible gold na hii ndio sababu ya inruders kuto kusumbua maeneo hayo kwa uvamizi.
Mgodi wa Tulawaka ulikua na visible gold na hii ilikua inapelekea hadi zaidi ya wangoni/intruders 1000 kuvamia RomPad (na ule ukanda wavamizi walikua wingi ni wanyantuzu na wasukuma.
Mgodi wa North Mara unakifusi madini chenye visible gold na hii ndio chanzo hasa cha wenyeji wa kule kuvamia kwasababu kazi kidogo pesa nyingi (hapa tunaongeza na ujeuri wao wa asili).
Kimsingi hakuna mlinzi wa mgodi anae ruhusiwa hata kumshambulia mvamizi na sheria inawataka wanapo waona wavamizi watoe taarifa kwa polisi ambao hufanya doria kwenye maeneo yoote ya mgodi nje na ndani ya uzio.
Kuhusu tegesha, yale ni mashamba ya wakazi ama wenyeji wa Nyamongo, Nyarero, Nyabichune, Kerende na kadhalika. Hivyo basi Barrick anapaswa kulipa fidia wenye mashamba/maeneo yao baada ya kufanya utafiti na kuona kama anapataka ili avune/achimbe dhahabu.
Mkuu hadi sasa maeneo yanayo julikaana North Mara anayamiliki rasmi ni Nyabirama na Gokona.
Upo nyonyo....🤔
Eneo la Murwambe mwekezaji alifanya tathmini tangu mwaka 2011 na akazuia uendelezqji wa ardhi ile. Miaka kumi baadaye anasema hana shida na eneo hilo hivyo wamiliki waendelee nayo. Dharau kubwa sana hii na serikali ipo. Unamzuia mtu kufanya shughuli zake kisha unajikuta tu hutaki maliyake, ndani ya miaka 10 ni maendeleo ama faida kiasi gani ingemletea.?
 
Mkuu trust me katika mambo yamelalamikiwa na watu hili ni mojawapo. Kwa ipande mmoja nakuunga mkono, upande mwingine napingana na wewe kidogo.

Mwekezaji alipoamua kusomesha vijana, mwanzoni tija ilionekana. Baadaye waliopewa dhamana ya kusimamia suala hilo wakaingiwa tamaa. Wakaanza kupeleka majina ya wasio wenyeji. Yaani jina mnaliona limetoka kijijini kwenu lakini huyo mtu hata hamumjui. Kifupi walianza kuuza nafasi.

Kuhusu wazazi kutosomesha ni ukweli usiopingika kwamba elimu sio kipaumbele. Hata madon wengi wa nyamongo wanathamini sana bar na guest houses kuliko ujenzi wa shule. Nyamongo kuna shule moja tu ya sekondari ambayo ni private na inafanya vizuri kwasasa inaitwa Maryo. Hii shule wakati inaanza ilipitia misukosuko mingi lakini mwanzilishi alisimama imara.

shule za msingi ambazo ni English medium ziko tatu mpaka sasa ambazo ni Pop John ii inayomilikiwa na kanisa katoliki, Nyamongo SDA hii inamilikiwa na kanisa la wasabato pamoja na maryo. Katika shule hizi zote, ni Pop John ndio kongwe na nyingine zote zimeanzishwa baada ya mwaka 2016. Hivyo suala la elimu sio kipaumbele huko.

Kwenye udokozi wa mali ya mwekezaji, ni kweli kabisa kwamba kijana akiajiriwa mgodini kwenye vitengo vya maana atafanya kila kitu kuhakikisha anaondokana na umasikini kwa kasi inayozidi mshahara wake. Matokeo yake vijana wameishia kuwa walinzi jamii ambao wanalinda maeneo ya nje ya mgodi jambo linalohatarisha usalama wao pia. Kitengo kingine ni upishi na usafi wa mazingirq. Lakini kumkuta kijana mzawa akiwa na kazi ya maana yenye mkataba wa kueleweka, ni wachache sana. Sababu kubwa ni tamaa.

Lakini pia kuna hao viongozi waandamizi wa usalama wilaya na mkoa, kwa kushirikiana na askari wasio waaminifu, wamewageuza intruders kuwa mtaji wao kwasababu intruder akikamatwa watahakikisha wanamkamua hadi waridhike ndipo aachiliwe. Kuna wakati mwekezaji alitenga eneo kwaajili ya kutupa mabaki ya mawe anayolipua, wenyeji walikuwa wanaenda wanazoazoa wanapata wanachopata. Baadaye askari waliowekwa kusimamia usalama wa hao raia, wakageuka majambazi wanaohakikisha huondoki na mali yako ikiwa umeneemeka na hauko miomgoni mwa mashushushu wao. Yani baadhi ya askari walikuwa na makundi ya vijana ambao wangepora mali kwa wengine na kushikiqna kwenye mgao na askari hao. Fujo ikatamalaki na ikawa sasa ni rasmi kuviziana na mapanga. Mwekezaji akaona isiwe taabu, akaamua kusitisha zoezi la kuwamwagia makapi (magwangala)

Back
Top Bottom