Nyani katema bungo ; Trump akubaliana na Putin Urusi kuingiza tani zake za Diesel Marekani na kwenye soko la Dunia

adriz

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2017
Posts
17,595
Reaction score
39,893
Moja kwa moja...

Kutokana na Vita vinavyoendelea kati ya Russia na Ukraine Marekani na mataifa ya Ulaya wakaiwekea vikwavyo vingi Russia mpaka kwenye Gas na mafuta yao . Marekani na Trump wakawa wakali kwa mataifa ambayo yalikuwa yanaendekea kununua mafuta ya Russia mfano mzuri ni India .

Kama tunavyojua Iran mambo yamekuwa magumu Marekani alivyotarajia umeenda kinyume na sasa Trump tumbo joto uchaguzi wa midterm elections mwezi wa 11 umekaribia huku wamarekani wakilalamika kupanda kwa nishati na gharama za maisha kutokana na Vita ya kujichagulia kuipiga Iran , na Sasa sio Marekani tu hali ni mbaya Dunia nzima.

Leo sasa Kuna habari hii Babu Trump kalegeza kwamba kwa Putin ili vyuma vikainikeπŸ‘‡πŸ‘‡

HABARI MPYA: Rais Trump amesema Urusi imekubali kutuma mamilioni ya tani za mafuta ya diseli kwenye soko la dunia kufuatia kile alichokiita mazungumzo "yenye mafanikio makubwa" na Vladimir Putin.
"Urusi itatoa mara moja zaidi ya tani 300,000 za Mafuta ya Diseli kwenye Soko la Marekani na la Dunia, tani zingine 500,000 wakati wa mwezi wa Novemba, na tani 1,000,000 mara baada ya hapo."
"Mbali na hilo, kulingana na hali ya Viwanda vyao vya Kusafisha Mafuta ya Diseli, Urusi itawasilisha, ndani ya muda mfupi, tani 3,000,000 za Mafuta ya Diseli." Trump anatabiri kuwa bei za diseli zitashuka kwa kiasi kikubwa na haraka, jambo ambalo litawafaidisha hasa wakulima, wafugaji, na madereva wa malori nchini Marekani.

#UziTayari
 
Inachekesha kama Sio raisi wako. Imagine wiki tatu nyuma kaipiga vikwazo now anaomba yeye. Wale waliopambania uraia wa marekani na kuupata kwa mbinde kama nawaona vile wanavyohaha jinsi house of cards inavyocolapse.
 
Trump na washauri wake ,walipga hesabu vibaya mno ktk hii vita ,,sijajua ni kwa nn Taifa kubwa kama marekani limeingia ktk vita ambao ndani ya VIONGOZI kama Trump ana majuto lakin kwa nje ni kama maharage yanayo rukaruka
 
Tangazo la Trump kwamba Putin atasambaza dizeli kwa Marekani, likiungwa mkono na Treasury waiver ya haraka inayosimamisha utekelezaji wa vikwazo dhidi ya Russia, linaonyesha mambo matatu kuhusu mahali ambapo vita yake dhidi ya Iran vimemfikisha.

Kwanza, madhara ya vita hivi alivyochagua mwenyewe (war of choice) yamevuka mipaka ya vituo vya mafuta vya Marekani na sasa yameingia kwenye uwanja wa siasa za kimataifa (geopolitical arena). Waiver hiyo itaendelea hadi Aprili 2027. Hii inakuja mwezi mmoja tu baada ya Trump kusaini sheria pana iliyolenga kuinyima Urusi mapato yake ya nishati. Uingereza na EU zinaendelea kushikilia vikwazo vyao, hivyo Washington imevunja msimamo wa pamoja na washirika wake. Zelensky alikiita kitendo hicho β€œa weak decision by strong partners” uamuzi dhaifu kutoka kwa washirika wenye nguvu. Trump amefikia hatua ambayo yuko tayari kuitoa Ukraine kafara na kudhoofisha mshikamano wa NATO, yote hayo kwa ajili ya kupunguza athari za kisiasa za ndani kuelekea uchaguzi wa midterm, zinazotokana na vita alivyoanzisha mwenyewe.

Pili, hatua hii inathibitisha kwamba madai yake kuwa Strait of Hormuz iko chini ya udhibiti wa Marekani si ya kweli. Kama mafuta kutoka Ghuba ya Uajemi yangekuwa yanapita kwa uhuru chini ya ulinzi wa Marekani, asingekuwa na haja ya kuipa Moscow concession ya kimkakati ili apate tani milioni chache za dizeli. Kamishna wa Ukraine anayeshughulikia vikwazo aliweka wazi jambo hilo: ikiwa kulegezwa kwa vikwazo dhidi ya Urusi kunasaidia kutuliza soko, basi mshtuko mkubwa wa soko ulitokana na vita dhidi ya Iran na blockade. Haukusababishwa na drones za Ukraine ambazo Trump alitumia wiki kadhaa kuzilaumu.

Tatu, inaonyesha jinsi ambavyo Trump anavyofanya maamuzi akiwa chini ya ushawishi mkubwa wa Israel. Njia mbadala ya kuizawadia Urusi kwa gharama ya washirika wa Marekani ilikuwa kufikia makubaliano ya haki na ya kudumu na Iran. Makubaliano hayo yangetambua haki na maslahi halali ya Iran, na kukubali kuishi pamoja kwa amani na taifa ambalo ni miongoni mwa mataifa muhimu zaidi katika eneo hilo. Lakini njia hiyo bado imefungwa kwa sababu ya shinikizo la pro-Israel lobby mjini Washington, pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje ambaye mshikamano wake wa kiitikadi na Israel ungefanya deal yoyote kama hiyo ife kabla haijafanikiwa. Kwa hiyo, Rais akaishia kwenda Kremlin akiwa na mkono ulionyoshwa kuomba dizeli.

Pamoja na yote hayo, amerudi akiwa amepata karibu hakuna kitu cha maana. Dizeli ya Urusi ni bandaid tu, siyo tiba ya tatizo. Mashariki ya Kati, si Urusi, ndiyo eneo kubwa zaidi duniani kwa export ya dizeli, na hakuna shehena ya dizeli kutoka Urusi inayoweza kuchukua nafasi ya supply ya Ghuba ya Uajemi ambayo vita hivi vimeikata. Na kwa upande mwingine anaingiza mafuta ya Iran kwake kupitia mgongo wa Russia

Kwa mujibu wa maelezo ya Trump mwenyewe, sehemu kubwa ya kiasi hicho cha dizeli kilichoahidiwa inategemea hali ya viwanda vya kusafisha mafuta vya Urusi (Russian refineries), ambavyo vinaendelea kushambuliwa na drones za Ukraine. Waiver hiyo itaisha mwezi Aprili, na wachambuzi tayari wanaonya kwamba kiasi cha dizeli kinachotarajiwa ni kidogo na huenda hata kisifike kabisa.

Madhara kwa Ukraine na mshikamano wa muungano wa washirika wa Marekani yatadumu kwa muda mrefu zaidi kuliko nafuu yoyote ambayo dizeli hiyo inaweza kuleta.

Marekani inatumia takribani tani 491,000 za dizeli kwa siku. Hivyo, tani 300,000 za dizeli ni sawa na mahitaji ya Marekani kwa takribani saa 14–15 tu.
Bila hata kutaja kwamba hizo β€œtani mpya” hazielekezwi zote Marekani; zinagawanywa kati ya Marekani na soko zima la dunia.
Bei ya mafuta haitashuka, na Urusi inapata ushindi rahisi wa kujijengea taswira nzuri kisiasa na mbele ya umma.

Suluhisho pekee la kumaliza upungufu huu wa mafuta ni kumaliza vita dhidi ya Iran.
 
USA kashikwa pumbu . gharama zimepanda ..Nchi ina uchumi mkubwa ila gharama tu yakuita Ambulance ni kubwa ,kuna vinchi hata top 20 havipo kwenye uchumi ila mambo kama hayo ni bure ..USA ni mashetani , sehemu ya kumwaga damu wanapeleka pesa kwa haraka bila hata congress's approval
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…