Nyani wamnyakua mtoto mikononi mwa mama yake, afariki dunia

Nyani wamnyakua mtoto mikononi mwa mama yake, afariki dunia

John7371

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2018
Posts
2,994
Reaction score
6,676
Kigoma. Kundi la nyani wa hifadhi ya Gombe iliyopo kijiji cha Mwamgongo wilayani Kigoma, limevamia nyumba ya Shayima Faya (20) na kumpokonya mtoto mchanga wakati akimnyonyesha na kutokomea naye porini ambapo baadaye mtoto huyo alifariki dunia.

Akizungumza leo Jumatatu Juni 20, 2022 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, James Manyama amesema tukio hilo limetokea Juni 18, 2022 katika kijiji hicho.

Amesema baada ya tukio hilo mwanamke huyo alipiga kelele kuomba msaada na majirani walijitokeza kumdhibiti mnyama pori huyo ambaye alimtupa mtoto huyo chini akiwa tayari amejeruhiwa kichwani, usoni na mguu wa kushoto.

"Wananchi walifanikiwa kulikimbiza kundi hilo la nyani lililomvamia mwanamke huyo wakati akimnyonyesha wanaye, na kufanikiwa kumpata mtoto akiwa amejeruhiwa lakini baada ya kufikishwa kituo cha afya Mwamgongo alifariki dunia,"amesema Manyama. Source- Gazeti la Mwananchi
 
Kwenye hili tukio kutakuwa na namna nyingine apa, nguvu za 'dark' zinahusika apa .................
 
kwenye hili tukio kulikuwa na namna nyingine apa, nguvu za 'dark' zinahusika apa .................
🤣 🤣 🤣 Pengine unaweza kuwa sahihi, ingawa hawa wanyama wana tabia sana ya kutowaogopa wanawake ikiwemo hata kuwapora vitu.
 
Huyu dada mpaka anapokonywa mtt na tumbili ilikuaje tena maajabu ya dunia haya
 
Hilo pori nyani wote wasakwe na wafyekelewe mbali na wananchi
 
Hilo ni tatizo la kuishi karibu na mbuga za wanyama,pole sana wafiwa...
 
dah inasikitisha sana...pole za dhati kwa dada
Inaumiza sana, hakuna jambo ambalo linachanganya kama kukutana na changamoto yenye athari kubwa halafu unakuwa helpless- unajikuta unashuhudia uharibifu machoni ila uwezo huna.
 
Back
Top Bottom