Nyanya za mshumaa/chungu/ngogwe za kukaanga

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363

Vipimo

Nyanya za mshumaa/chungu 20 kiasi

Kitunguu 1

Nyanya/tungule 2

Mafuta ya zaytuni (olive oil) 3 vijiko vya supu

Pilipili mbichi 1

Kitunguu saumu(thomu/galic) 3 chembe

Chumvi kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Osha nyanya za mshumaa/chungu kisha zichemshe kidogo.

  1. Mwaga maji, menya maganda na ukatekate vipande vipande.

  1. Katakata kitunguu, nyanya vipande vidogovidogo (chopped)

  1. Saga au katakata pilipili mbichi na thomu.

  1. Weka mafuta katika sufuria, tia vitu vyote pamoja. Kaanga kwa muda huku unakoroga hadi iwive.

  1. Pakuwa katika chombo, nyunyizia mafuta ya zaytuni.
 
Mhh hizi ngogwe zipikwe na bamia la kukoroga ulichanganye na duvi au kiji nyanya kwa mbali uchome na kipande cha papa au umchanganye na bamia au hata bamia uliweke magadi kidogo na ugali wa kumix (dona) ntakula unisahau nyanya chungu peke yake hapana kabisa hazipandi MziziMkavu
 
Unazipenda Mama mkwe farkhina Nyanya chungu? ngojea tumuita naye Mkuu utafiti na Mkuu BAK waje kuthibisha uzuri wa nyanya chungu njooni haraka munaitwa huku.
 
Last edited by a moderator:
Unazipenda Mama mkwe farkhina Nyanya chungu? ngojea tumuita naye Mkuu utafiti na Mkuu BAK waje kuthibisha uzuri wa nyanya chungu njooni haraka munaitwa huku.

Kwa kweli binafsi sizipendi kuna siku aunt yangu alitupikia mchuzi wa biringanya akasaga sikula kwa kweli nilihis sjui nakula kitu gani
 
Duh. mbona kunitoa mate mwenzio? hiyo kitu sijaipiga looong time, hapa nawaza huyo papa ntamtoa wapi keshooo...sio vidhuriii hivoooo....
 
Mie nazipenda sana ziwekwe kwenye matembele/mchicha. Hata kwenye samaki iliyoungwa kwa nazi huwa bomba sana.

Unazipenda Mama mkwe farkhina Nyanya chungu? ngojea tumuita naye Mkuu utafiti na Mkuu BAK waje kuthibisha uzuri wa nyanya chungu njooni haraka munaitwa huku.
 
Duh. mbona kunitoa mate mwenzio? hiyo kitu sijaipiga looong time, hapa nawaza huyo papa ntamtoa wapi keshooo...sio vidhuriii hivoooo....

ahaha ungekua karibu huku ningekuletea mana wanapatikana kwa wingi huku
 
Izo kwenye picha si tunguja kwetu tunaita ivo alafu haziliwi...
Mrs Kharusy na Angel Nylon
 
Last edited by a moderator:

Madame S umenikumbusha kwetu Tanga loooh, kwa bibi hapo nilikua natamani kula kila siku....mlenda wa bamia, papa na ugali...chini ya mwembe ukimaliza washushia na maji baridiiiiiiiiiiiii.
 
MziziMkavu izo kwende picha ndulele sikujua kama zinaliwa,,,,
 
Madame S umenikumbusha kwetu Tanga loooh, kwa bibi hapo nilikua natamani kula kila siku....mlenda wa bamia, papa na ugali...chini ya mwembe ukimaliza washushia na maji baridiiiiiiiiiiiii.

Na ndo nilipo tanga yaani papa sjui nguru mtaaAmu
 
Na ndo nilipo tanga yaani papa sjui nguru mtaaAmu

Kuna mtu kasafiri huko juzi nimetuma aniletee papa akija....cant wait kupika na nazi na ugali wa mhogo, tamu balaa.
 
Na ndo nilipo tanga yaani papa sjui nguru mtaaAmu

Kuna mtu kasafiri huko juzi nimetuma aniletee papa akija....cant wait kupika na nazi na ugali wa mhogo, tamu balaa.
 
ndo dawa ya mambo yetu yale au?
 
Madame S si bure utakuwa na asili ya Tanga.
Dah! umenikumbusha mbali sana.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…