Hoja za jaji naona zina msingi, kwa sababu kama hao kina Halima walipeleka affidavit zao [viapo] kwa kina Kibatala, ili kujibu kilichoandikwa kwenye affidavit hizo [counter affidavit] lazima ingechukua muda.
Naona jaji ametoa wiki mbili kwa hayo mazoezi yote kukamilika kabla ya shauri la msingi kuanza kusikilizwa tarehe 13.06.2022.
Kwangu suala la msingi ni kuwa sioni popote hapo kwenye maamuzi ya jaji wakina Mdee walipoomba wasiondolewe uwanachama wao Chadema.
Sasa Spika alikubaliana vipi na sababu ya kina Mdee kufungua kesi mahakamani bila kujua nini walichoiomba mahakama?
Hawa kina Mdee wanaomba waendelee kuwa wabunge kulingana na hayo majibu ya jaji [kifungu cha 1], sasa vipi waendelee kuwa wabunge kama uwanachama wa chama cha siasa hawana kulingana na Katiba?