Ubaya Ubwela
JF-Expert Member
- Jul 24, 2024
- 3,014
- 7,343
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu imetajwa leo, Jumatatu Septemba 08.2025 kwa mara ya kwanza kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam chini ya jopo la Majaji watatu (3) wakiongozwa na Jaji Ndunguru
Kabla ya kesi hiyo kuanza kusikilizwa mshtakiwa ambaye anajitetea mwenyewe aliwasilisha Mahakamani hapo mapingamizi, akipinga utaratibu utaratibu wote uliotumika kuanzia kukamatwa kwake wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma hadi kesi ilivyoendeshwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kutokana na kile alichosema kuwa taratibu za kisheria zimekiukwa
Sambamba na hilo Lissu ambaye ni Mwanasheria na Wakili kitaaluma amesema nyaraka aliyokabidhiwa kutoka upande wa Jamhuri kuhusiana na kesi hiyo zinakinzana na nyaraka zilizowasilishwa kwenye mifumo wa Mahakama