Nyaraka za Nazi Zagunduliwa Kwenye Mahakama Kuu Argentina

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Miaka zaidi ya themanini tangu utawala wa Adolf Hitler ulipoanzisha vita vya dunia na mauaji, kivuli cha historia ya Nazi kimeibuka tena, safari hii kutoka kwenye sehemu isiyotarajiwa, basement ya Mahakama Kuu nchini Argentina

Historia ya Nazi ilianza mapema miaka ya 1930, pale chama hicho kiliponyakua madaraka nchini Ujerumani chini ya uongozi wa Hitler. Kikiwa na itikadi ya ubaguzi wa rangi na utawala wa mabavu, chama hicho kilianzisha Vita ya Pili ya Dunia mwaka 1939, vita ambavyo vilisababisha vifo vya mamilioni ya watu duniani kote, ikiwa ni pamoja na Wayahudi milioni sita waliouawa katika Holocaust

Baada ya Ujerumani kushindwa mwaka 1945, baadhi ya viongozi wa Nazi walikimbilia nchi mbalimbali, na Argentina ikawa mojawapo ya maeneo yao salama. Jamhuri hiyo ya Amerika Kusini iliwapokea kwa mikono miwili baadhi ya wahalifu wa kivita, akiwemo Adolf Eichmann, aliyekamatwa baadaye na maafisa wa Israel akiwa anaishi kwa siri mjini Buenos Aires.

Hivi karibuni, kivuli hicho cha historia kimegonga tena vichwa vya habari baada ya kugunduliwa kwa masanduku yenye nyaraka halisi za Nazi, yaliyokuwa yamehifadhiwa kwa miongo kadhaa kwenye ghala la chini ya ardhi la Mahakama Kuu ya Argentina.

Eliahu Hamra, rabi wa kituo kikuu cha jamii ya Wayahudi nchini Argentina, anakumbuka kupokea simu usiku mmoja mwishoni mwa mwaka kutoka kwa Silvio Robles, Mkuu wa Utumishi wa Rais wa Mahakama Kuu. Robles alitaka ushauri kuhusu jambo nyeti – walikuwa wamegundua masanduku zaidi ya kumi yaliyosheheni nyaraka za utawala wa Hitler.

Ndani ya masanduku hayo kulikuwa na picha za Hitler, vitambulisho vya uanachama wa mashirika ya kazi ya Nazi vilivyokuwa na mihuri ya swastika, pamoja na nyaraka nyingine za kikazi na kiutawala kutoka zama hizo za giza.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mahakama Kuu, nyaraka hizo ziliingia nchini Argentina mwaka 1941 kupitia meli ya Kijapani. Zikiwa sehemu ya mizigo 83 kutoka ubalozi wa Ujerumani ulioko Tokyo, zilizuiwa na maafisa wa forodha wa Argentina kwa kuhofia zingeathiri msimamo wa nchi huo wa kutoshiriki vita

Wakati huo, Argentina ilikuwa na idadi kubwa ya wazungumzaji wa Kijerumani – takribani 250,000. Mwaka 1938, baada ya Hitler kuimeza Austria, zaidi ya watu 10,000 walikusanyika kwenye uwanja mjini Buenos Aires kusherehekea tukio hilo, hali iliyowatisha na kuwashangaza wananchi wengi wa kawaida. Ingawa serikali ya Argentina ilivunja tawi la chama cha Nazi nchini humo mwaka 1939, athari na mitazamo ya ki-Nazi iliendelea kuishi kwa njia ya chinichini

Kwa jamii ya Wayahudi nchini humo, tukio hili ni kumbukumbu chungu lakini pia fursa ya kuibua mjadala wa ukweli. Nyaraka hizi, ambazo zimefichwa kwa muda mrefu, sasa zinaibua maswali mazito kuhusu historia ya taifa hilo na nafasi yake katika kuwahifadhi watenda maovu baada ya vita

===

The Supreme Court official had a secret to share when he called Eliahu Hamra, the rabbi of Argentina's main Jewish community center, one night around the turn of the year

The court had found a dozen boxes of Nazi documents in its basement archive containing photos of Hitler as well as thousands of red Nazi labor organization membership booklets stamped with the swastika of the Third Reich. Silvio Robles, chief of staff to the court's president, wanted the rabbi's advice about how to handle the discovery, Hamra recalled

NAZI.png

Source: Reuters
 
Inasikitisha sana
 
Kuna story ya U-boats mbili (U-530 and U-977) kuingia Argentina baada ya kuanguka utawala wa kinazi, kulikuwa na hofu huenda hizo U-boats moja wapo ilimbeba Adolph Hitler na baadhi ya maafisa yake wakikimbilia Argentina.

ndani ya mitaa ya Damascus - Syria.
 
ikiwa ni pamoja na Wayahudi milioni sita waliouawa katika Holocaust
Hii ya wayahudi Million 6 kuawa ilikuwa kete ya kisiasa ila sio kweli kimantiki, ilikuwa kete ili kulata uhalali wa kupewa eneo lao na ulimwengu uwaonee huruma.
 
Back
Top Bottom