Nyaraka za Siri za Mali za Kifamilia zina hifadhiwa wapi?

Unaweza kuziweka kwa mwanasheria, benki au mahakamani. Ni sehemu salama kwa kutunza nyaraka kama hizo hasa, wosia.
 
Serikalini panaweza kuwa mahali salama pakuhifadhi nyaraka, lakini ni vzuri mkafanya utaratibu zikawa pia kwenye form ya soft copy

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh hii point ndio sijswahi kuielewa 'watu kugombania mali za mtu aliyefaliki".

Hivi kama mnaamini katika dini mnadhani mzee wenu anaweza kupumzika kwa amani kama vita zinaendelea kwenye familia kisa mali alizotafuta kwa nguvu zake..

Btw mnaweza kutafuta mwanasheria atawapa ushauri jinsi ya kifanya hapo.
 
Umeongea kinyume chake, kama wanaamini dini watajua kuwa kupumzika kwa amani au vinginevyo hakuathiriwi na lolote linaloendelea huku bali matendo ya marehemu alipokuwa hai
 
RITA ndo wanatoa huduma ya kuhifadhi nyaraka hasa za mirathi
 
Mzee kafariki watoto wote wanapigania mali, madhara ya familia (two-in-one) hayo. Acheni ubahili, tafuteni mwanasheria awape ABC za namna ya kutatua matatizo ya familia.

Lakini pia, kila mmoja wenu afanye kazi ili amiliki mali zake binafsi(sorry nimetoa ushauri japo hukuutaka)
 
RITA ndo wanatoa huduma ya kuhifadhi nyaraka hasa za mirathi
 
Umeongea kinyume chake, kama wanaamini dini watajua kuwa kupumzika kwa amani au vinginevyo hakuathiriwi na lolote linaloendelea huku bali matendo ya marehemu alipokuwa hai
Sasa wazee wa dini wanapomuombea marehemu au zile ibada za mazishi huwa zinasaidia nini??
 
kwa mganga mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…