Nilimsikia waziri husika akisema wataweka nyasi za asili, ilimechi za kimataifa kama AFCON ichezwe kwenye viwanja hivyo
"Katika kuhakisha Tanzania inaandaa mashindano ya Kimataifa na kikanda, Serekali imetenga Mwaka huu wa fedha 2022/23 kiasi cha Shilingi Bilioni 10, kukarabati viwanja.
Kwa hatua ya kwanza vitaanza
viwanja saba (7) vilivyopo katika Majiji, ambavyo ni Jamhuri – Dodoma, Sheikh Amri Abeid - Arusha, Sokoine - Mbeya, CCM
Kirumba – Mwanza, na Mkwakwani - Tanga.
Aidha, ukarabati huo utavihusisha viwanja vya
Uhuru na Benjamina Mkapa Jijini Dar es Salaam. Hatua ya pili ni kukarabati viwanja vingine ikiwa ni pamoja na kuweka nyasi
bandia na majukwaa katika mikoa ya Kigoma, Rukwa, Mtwara, Iringa, Tabora na Shinyanga baada ya kujadiliana na wamiliki wa viwanja hivyo.
Mkakati huu utaiwezesha Tanzania kufanikisha maandalizi ya kuwa mwenyeji wa mashindano ya AFCON ambayo tayari Tanzania imependekezwa kwa mwaka 2027 ambayo ni ndoto ya Rais, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ya kuandaa mashindano ya AFCON