JS Dairy Farm
JF-Expert Member
- Feb 13, 2022
- 331
- 744
Nyasi za Juncao ni nyasi/majani yaliyofanyiwa utafiti nchini China.Utafiti ulifanywa na Profesa Zin Zhanxi wa chuo kikuu cha Fujian Agriculture and Forestry ni hybrid ya aina tofauti za Napier na yanafanana na majani tembo(elephant grass)Yanafahamika pia kwa majina ya Giant Juncao, majani ya fangasi na majani ya maajabu.
China wanayatumia zaidi kwa ajili ya kutengenezea uyoga.
Maajabu yake:
Ni nyasi kubwa,ndefu na pana,urefu unaweza kufika futi 8,yana mizizi imara na mirefu inayofanya yavumilie ukame,hutoa machipukizi mengi,yanakua kwa haraka, yanastawi sehemu za hali ya hewa ya baridi na joto, yanastawi sehemu za mazingira mbalimbali.
Yana virutubisho vya wanga, vitamin na kiwango cha protini ni 12%.Eka moja ya Juncao huweza kutoa tani 180-200 za majani mabichi kwa mwaka mmoja na hivyo kutosha kulisha ng'ombe 15 kwa mwaka,yaani ukipanda Juncao kwenye eka moja utaweza kulisha ng'ombe 15 kwa mwaka mmoja.
Nyasi hizi zimeanza kupandwa Afrika na nchi mbalimbali za Asia na Tanzania pia zipo,mwaka 2017 nchi ya Papua New Guinea iliyopo Asia iliweka rekodi ya kuvuna tani 341.6 kwenye eka moja na hicho ndicho kiwango kikubwa cha mavuno ya Juncao kilichorekodiwa hadi Sasa.
Pia ni nyasi ambazo zinatumika kulisha kuku na ndege wengine wanaokula majani kama chakula cha ziada.
Kwa maelezo zaidi juu ya malisho ya wanyama kama ng'ombe,punda,mbuzi na kondoo soma kitabu cha Malisho bora ya wanyama wanaokula nyasi.
Kitabu ni cha Softcopy, bei 5000.
Mawasiliano:0756625286.
View attachment 2234366