Nyasi za Juncao: Suluhusho la malisho ya ng'ombe, mbuzi na kondoo

Nyasi za Juncao: Suluhusho la malisho ya ng'ombe, mbuzi na kondoo

JS Dairy Farm

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2022
Posts
331
Reaction score
744
Nyasi za Juncao ni nyasi zilizofanyiwa utafiti nchini China, utafiti ulifanywa na Profesa Zin Zhanxi wa chuo kikuu cha Fujian Agriculture and Forestry.Ni hybrid ya aina tofauti za napier na yanafanana na majani tembo(elephant grass).Yanafahanika pia kwa majina ya Giant Juncao na majani ya maajabu.China wanayatumia zaidi kwa ajili ya kutengenezea uyoga.

Maajabu yake:
Ni nyasi kubwa, ndefu na pana, urefu wake unafika futi 8,Yana mizizi imara na mirefu inayofanya yavumilie ukame,hutoa machipukizi mengi,yanakua kwa haraka.

Nyasi za Juncao pia zina virutubisho vya wanga, vitamin na kiwango cha protini ni 12%.Eka moja ya Juncao huweza kutoa tani 180-200za majani mabichi kwa mwaka mmoja kiasi kinachotosha kulisha ng'ombe 15 kwa mwaka mmoja.

Mwaka 2017 nchi ya Papua New Guinea iliweka rekodi ya kuvuna tani 341 kwenye eka moja na hicho ndicho kiwango kikubwa cha mavuno ya Juncao kilichorekodiwa hadi sasa.

Juncao pia huweza kulisha kuku na ndege wengine wanaokula nyasi kama chakula cha ziada.

Tupande nyasi ili tuepukana na ukosefu wa malisho hasa wakati wa ukame.
Ukihitaji mbegu za Juncao piga simu-:0756625286.
Bei Kg Tsh.5000.(elfu Tano tu).

.
Screenshot_20220702-103059_1.jpg
IMG_20220625_064632_167.jpg
Screenshot_20220702-181035_1.jpg
IMG_20220702_093340_878.jpg
IMG_20220702_093340_878.jpg
 
Bado tuko nyuma sana kuliko wenzetu kwa Kweli
Viongozi wetu na sisi wenyewe hatujishughulishi na kuungana na dunia
Huu mmea hapo jirani Kwa Zulu natal mwaka 2010 walikuwa wamepanda sana

Hata Rwanda pia wamepanda sana ila sisi tunaisaidia dunia bila kujijua huku wakibeba mbegu na hata wadudu na wanyama ila sisi haturudi na kitu kipya pindi tunapokuwa nje ya mipaka
 
Mbona ni SAwa na majani ya mabingo bingo tu
 
Bado tuko nyuma sana kuliko wenzetu kwa Kweli
Viongozi wetu na sisi wenyewe hatujishughulishi na kuungana na dunia
Huu mmea hapo jirani Kwa Zulu natal mwaka 2010 walikuwa wamepanda sana

Hata Rwanda pia wamepanda sana ila sisi tunaisaidia dunia bila kujijua huku wakibeba mbegu na hata wadudu na wanyama ila sisi haturudi na kitu kipya pindi tunapokuwa nje ya mipaka
Hata TANZANIA haya majani mbona yapo.
 
mbegu zinapatikana Kibaha,mtu anayehitaji tuwasiliane 0756625286,yanatumwa sehemu yoyote ya Tanzania.
Ni nyasi zinazotoa malisho mengi katika eneo dogo.Zinafanana na majani tembo lakini zenyewe ni matokeo ya mchanganyiko wa napier tofauti tofauti.
 
Hapana wewe unazungumzia majani tembo/elephant grass au mabingobingo haya ni tofauti yanafanana kwa muonekano na majani tembo ila Juncao yana sifa ya ziada kama kutoa machipukizi mengi kwa kipindi kifupi,majani yake ni marefu na mapana,kutoa malisho mengi yanayoweza kufika tani 200 kwa mwaka kwenye eneo la ukubwa wa eka moja.
Ukanda wa tukuyu yapo miaka mingi
 
Hapana
Bado tuko nyuma sana kuliko wenzetu kwa Kweli
Viongozi wetu na sisi wenyewe hatujishughulishi na kuungana na dunia
Huu mmea hapo jirani Kwa Zulu natal mwaka 2010 walikuwa wamepanda sana

Hata Rwanda pia wamepanda sana ila sisi tunaisaidia dunia bila kujijua huku wakibeba mbegu na hata wadudu na wanyama ila sisi haturudi na kitu kipya pindi tunapokuwa nje ya mipaka
, Serikali ina mchango mkubwa,kwani bila Serikali mbegu ya Juncao isingefika kutoka China.
 
Hapana

, Serikali ina mchango mkubwa,kwani bila Serikali mbegu ya Juncao isingefika kutoka China.

Tunachelewa sana hata mtu wa kawaida anaweza kuleta
Wazungu wanachukua mpaka vipepeo na tunawaacha wanabeba tu
Sio kwa ubaya ila ni lazima twende na wakati
Angalia mbuzi wa Boer wapo South Africa lakini ukiulizia bongo utaishia kuibiwa tu
Ila wamejaa Uganda na Kenya

Tunahitaji maendeleo ila sio baada ya miaka 20 ndio tunashtuka na kitu
 
Back
Top Bottom