Nyayo za miguu kuwa ngumu sana

Nyayo za miguu kuwa ngumu sana

DASA

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2011
Posts
1,031
Reaction score
302
Jamani unyayo wangu ni mgumu sana kiasi kwamba nikikugusa naweza kukuchuna kabisa na kukutoa damu, nimejaribu kuangalia nyayo za watu wengine naona ni laini sana ukilinganisha na zangu, sasa hii imekuwa ikininyima raha hasa ninapokuwa na mamsap kitandani maana wakati mwingine huwa namuumiza kwa bahati mbaya.

Je ni ukosefu wa kitu fulani mwilini! au tatizo ni nini!!.
 
Unavaa viatu? kama huvai nayo inaweza kuwa sehemu ya tatizo (kuleta magaga) jaribu pia kusugua miguu na kupaka asali,nilishawahi kujaribu na kufanikiwa.watakuja wataalamu waongezee
 
inaelekea ukiwa mtoto ulikuwa unasakanya sana....jaribu kufanya pedicure(the real one) mara kwa mara.....na uepuke kuvaa sandals muda mwingi....raba ndio tiba mbadala wa tatizo lako....
 
Jamani unyayo wangu ni mgumu sana kiasi kwamba nikikugusa naweza kukuchuna kabisa na kukutoa damu, nimejaribu kuangalia nyayo za watu wengine naona ni laini sana ukilinganisha na zangu, sasa hii imekuwa ikininyima raha hasa ninapokuwa na mamsap kitandani maana wakati mwingine huwa namuumiza kwa bahati mbaya.

Je ni ukosefu wa kitu fulani mwilini! au tatizo ni nini!!.

Haina neno kama wewe ni mkaka, ila kama ni Mdada hiyo ni hatari
 
chukua ile ya kusugulia miguu watembezayo machinga.mtu akusugue kila wiki mara moja.baada ya kusugua osha kisha paka lotion ya miguu au yoyote.mbona utapenda kumgusa memsap bila woga.
 
Jaribu kuwa unaisugua, afu paka mafuta ya Nivea asubui na jioni. Kumbuka kuvaa viatu vya kufunika.
 
Weka maji ya moto kwenye beseni, tia chumvi kidogo na sabuni ya maji kisha tumbukiza miguu yako uache ikae humo mpaka ukigusa hivi na kucha unaona ngozi ya juu inatoka kama unga. Baada ya hapo chukua jiwe, au kikwangulio cha chuma kama unacho usugue mpaka ukigusa na kuvha hamna kinachotoka. Kisha suuza vizuri,kausha alafu paka mafuta.

Baada ya hapo kua unasugua kila ukioga.
 
Thanks all, Ila kazi ninayo.
 
Kwetu niliwahi kulisikia hilo tatizo huwa linaitwa 'mbuachi'
tiba yake ilikuwa huo unyayo unaupaka mafuta ya nazi kisha
unakanyaga kwenye figa lenye moto. unarudia rudia baada ya
muda fulani nyama italainika, sasa kwa huku mjini sijui figa utapata wapi,
ila pole sana.
 
Back
Top Bottom