Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
DKT. Magufuli akiwa anaendelea na kampeni za uchaguzi 2020, amepita kijiji cha Nyehunge akiwa anaelekea Geita ambapo kutoka Sengerema mpaka Nyehunge ni kilomita 46. Alisimama kuongea na wananchi waliokuwa wakimsubiri barabarani, wakati anaielezea barabara hiyo ghafla aliomba simu yake na kumpigia mtu ambae baadae alijulikana ni mkurugenzi mkuu wa TANROADS, Injinia Mfugale na mazungumzo yao yalikuwa hivi.
Magufuli: Hallo, Chief executive
Mfugale: Naam mheshimiwa Rais
Magufuli: Hujambo
Mfugale: Sijambo mheshimiwa
Magufuli: Uko wapi?
Mfugale: Niko Dar es Salaam TANESCO tunazungumzia habari ya Nyerere dam.
Magufuli: Haya, sasa mimi niko Nyehunge, kutoka Sengerema mpaka Nyehunge ni kilomita 46, hii barabara tumeshaifanyizia feasibility study na detail design, nimesimama hapa na wananchi, nataka hii barabara, mimi si ndio Rais?
Mfugale: Ndio mheshimiwa(Wananchi kicheko cha furaha)
Magufuli: Nyehunge Oyee, Unanielewa Chief? Basi hii barabara uitangaze kwa ajili ya kuijenga kwa kiwango cha lami. Huu ni mwezi wa ngapi? (Mfugale: Mwezi wa tisa). Haya uandae document zote kabla ya mwezi wa 12 haujafika na kandarasi apatikane, niulize hela nitazitoa wapi. Sawa Mfugale?
Mfugale: Nimekuelewa mheshimiwa Rais
Magufuli: Umenielewa, mueleze na Waziri kwamba hayo ni maagizo yangu wala yasibadilike, Asante sana.
MWISHO WA MAONGEZI