"Lakini hata shida hizi ziweje kwa ukubwa, zaweza kuondolewa. Shida zenyewe ni kama miguu ya jongoo tu. Mtoto wa jongoo alimwuliza mama yake: "Mama, mbona nina miguu mingi, je nianze kwenda kwa mguu au miguu ipi?" Nasi hapa tulitoe jibu hilo hilo la mama jongoo kwa mwanawe : "Nenda mwanangu, nenda tu”.