Nyerere aliwahi sema “Nilitegemea majitu yenye nguvu ndani ya CCM yangehamia upinzani ili kupambania mabadiliko ya nguvu”

mavumbi

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2013
Posts
596
Reaction score
328
1. RIP kwa wote waliotangulia, miongoni mwa watu maarufu na wenye ushawishi / mvuto
  • Mrema alihamia upinzani kwa shinikizo la Mwl Nyerere
  • Sumaye alihamia upinzani kutafuta umaarufu alioukuwa akiendelea kuutamani
  • Lowasa alienda kwa kusukumwa na tamaa yake ya Urais
  • Kingunge alihamia huko kufukuzia umaarufu wa uzeeni - alikuwa wapi huko nyuma?
  • Membe aliwakimbia wana CCM wenzie akijua hakubaliki - hadi kuwekewa vikao na CCM
  • Nyalandu alikimbia baada ya kuona mwelekeo unataka kumtafuna kwa madudu yake serikalini.
Wote ilikiuwa maslahi tu. 90% wakarudi CCM, ukiacha Mrema aliyekuwa na mahesabu yake
2. Na huko kwenye upinzani
  • Lipumba kayumba yumba hadi kuyumbisha Chama
  • Walid Kabouru wapi – CCM
  • Hata Masumbuko Lamwai?
3. Nyerere aliwahi sema “Nilitegemea majitu yenye nguvu ndani ya CCM yangehamia upinzani ili kupambania mabadiliko ya nguvu” - maana aliona ili nchi ipige hatua mbele ni lazima kuleta mabadiliko ya msingi ambayo yeye asingeweza kuyaongoza . Lakini hata hivyo, WaTz na hasa wana CCM kwenye nafasi za ushawishi wakawa waoga.

4. Ndio maana MAGUFULI akajijengea umaarufu – na tutaendelea hivyo hadi aje MAGUFULI mwengine ndani ya CCM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…