Adolf Mark
Member
- Nov 4, 2011
- 50
- 26
Nimepitia kitabu cha kanisa katoliki kinachoelezea historia za watakatifu, kwa nchi za Afrika Mashariki nimeona mashahidi wa uganda pekee kama karoli lwanga, mathias mulumba n.k, na kwa majirani zetu wa sudan nimemwona sista josephine bakhita ambaye baadaye aliishi italia, kongo nimemwona isdore bakhanja, lakini kenya, tanzania, msumbiji, rwanda sijaona yeyote, hata ivyo kutoka jimbo la musoma nimepata taarifa kuwa vatican ipo kwenye mkakati wa kumcanonize nyerere, naamini hayati mwl nyerere atakuwa mtakatifu wa kwanza kutoka Tanzania, bila shaka itaongeza heshima ya kanisa la Mungu Tanzania.