Tarehe 14/10 Kila mwaka ni siku kubwa na ya kukumbukwa nchi Tanzania,ni siku ambayo Watanzania hawatoisahau kwa kuondokewa na aliyekuwa kipenzi chao na mtoboa siri mkubwa kwa mambo yaliyo nyuma ya pazia.Mwalimu hakuwa mnafiki,muoga wala mzandiki katika kuhakikisha ana simamia maslahi ya taifa.
Mengi yamesemwa na yataendelea kusemwa kila kukicha lakini ukweli utabaki pale pale kuwa yeye ndiye father of the Nation.Kauli zake,vitendo vyake na nia yake vilitosha kumtofautisha na viongozi mbalimbali katika dunia hii.Mwalimu hakuwa na makuu na ndiyo maana siku hii ya kumkumbuka ilitakiwa iwe ni siku maalum ya kujichunguza na kujiangalia kama kweli tunasimamia yale aliyotuasa katika kusuma gurudumu la maendeleo mbele.
Siku hii itakuwa na maana zaidi ikiwa tutatekeleza kwa vitendo vya ambayo mwalimu aliyaona yana tija kwa mustakabali wa maendeleo ya taifa letu.Ni zaidi ya muongo mmoja tangu atutoke lakini Tanzania imekuwa tofauti na hali aliyoiacha,utadhani aliondoka miaka 50 iliyopita.
Rushwa imeshika hatamu,matajiri ndiyo walioukumbatia uchumi wetu.Matabaka yanaongezeka siku hadi siku pato la kima cha chini cha mshara ratio yake kwa wastani ni zaidi ya1:60.Mfumuko wa bei kila kukicha,hakuna wakumuogopa mtu,kila mmoja ana peleka mambo yake atakavyo ila mbaya zaidi wanao umia ni maskini walalahoi.
tunakwenda kumuenzi kwa ushujaa mkubwailihali nchi imeuzwa kwa wageni,hata wale makaburu ambao tuliwaimba sana kama maadui wa haki za kibinadamu ndiyo walio shikiria uchumi wetu.Wameuza mpaka zile benki za makabwela na kuliulia mbali lileshirika letu la ndege ATC.
Kumbukumbu hizi zingeleta tija pamoja na gharama za maandalizi yanayofanywa huko mkoano Shinyanga kama tungeyakataa yale yote ambayo ni adui wa maendeleo ya taifa letu.Mwalimu aliwahi kusema kuwa tunao maadui wakubwa watatu,njaa,maradhi,umasikini na ujinga.Lakini maadui wetu hao leo hii wamegeuzwa deal.Tunashuhudia madawa fake yanayotengenezwa na kiwanda chetu cha madawa,tumeona jinsi mbolea inavyochakachuliwa kwa mtindo maarufu wa mbolea za voucher.Mitaala ya elimu kila siku ina chakachuliwa hali iliyosababisha watoto wetu kupata bora elimu.
Rushwa imegeuzwa takrima,nchi inaendeshwa kisanii lakini leo tunatumia kodi za wanyonge kuundaa sherehe kubwa zilizo chini ya mwamvuli wa kumuenzi mwalimu.Si ajabu ukichunguza ndani yake utakuta gharama hewa zimejaa katika maandalizi hayo.
Wapi tunaelekea wapi ikiwa mwalimu hakuwa muumini wa haya yote yaliyojaa nchini mwetu kama kukithiri kwa ufisadi,rushwa kutamalaki na uwizi wa kimachomacho katika halimashauri zetu.Umoja wa kitaifa umepotea,leo watu wana jadili udini,ukabila na ukanda.Wananchi walijivunia Utanzania wao lakini leo watu wana jinasibu kwa dini na makabila yao.
Familia imekuwa ndizo zina milki ikulu na hata kufikia kutoa amri kwa vyombo vya dola bila hata kuogopa,si ajabu leo ukasikia mtoto wa Kiongozi fulani ana toa amri kwa vyombo vya dola aidha kwa kuwa tu baba au mama ni kiongozi fulani ndani ya nchi.
Taasisi za kibenki zinatishwa na wafanya biashara kwa kuwa wana mawasilianao na ikulu,lakini ikifika siku hii Watanzania wakiungana na viongozi wao wana kaa pamojandani ya uwanja mkubwa na kuthubutu kusema wana muenzi Mwalimu.Tanzania yetu itasonga mbele ikiwa tukiacha unafiki na sifa za kijinga ilihali hatutendi kutokana na sifa tunazo mtunukia kiogozi fulani