Nyerere Day 2022: Mwalimu na Edouard Masengo 1958

Nyerere Day 2022: Mwalimu na Edouard Masengo 1958

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
NYERERE DAY 2022: EDOUARD MASSENGO ALIPOKUTANA NA JULIUS KAMBARAGE NYERERE

Jioni hii rafiki yangu moja kutoka Ulaya kanipitia kunijua hali na kaniletea CD ya muziki wa Edouard Masengo na Mwenda Jean Bosco.

Ikawa kanikumbusha kuwa Masengo alipata kuja Dar es Salaam wakati akiwa katika kilele cha ufanisi wake katika muziki wakati huo anaishi Nairobi.

Nikamwadithia kidogo historia ya Masengo.

Hayo hapo chini nimetoa katika mswada wa kitabu kuhusu maisha ya Ally Sykes:

''Peter Colmore signed Edouard Masengo the gifted guitarist from Elizabethville, Belgian Congo to promote Coca-Cola.

Masengo had come to Nairobi with a group called Je-Co-Ke meaning, Jean Comedian Katanga.

Colmore who was already in broadcasting was informed that there was a young man in town who played terrific guitar.

Colmore went to the hotel where Masengo was lodging. There he found Masengo in a dirty hotel at River Road.

He was sitting on the floor playing his guitar with people around him listening to his music.

This was the beginning of the association between Colmore and Masengo.

There was the famous poster of Masengo with his guitar and holding a bottle of Coca-Cola.''

(''Under the Shadow of British Colonialism...'')
Ally Sykes and Mohamed Said

Hakuna siku ambayo itaweza kupita usisikie muziki wa Eduardo Masengo katika radio.

Nalikumbuka tangazo lake akitangaza Coca Cola.

Nilikuwa nikipita Mtaa wa Swahili na Kitchwele (sasa Uhuru) kabla ya kufika Swahili na Stanley (sasa Max Mbwana) upande wa kushoto kulikuwa na duka la Muhindi nje ndipo lilipokuwapo tangazo la Eduardo Masengo.

Nilikuwa navutiwa sana na tangazo lile.

Lile koti la mistari alilovaa Masengo na guitar aliloshika vilivutia akili yangu ya kitoto.

Ally Sykes na Julius Nyerere walikuwa marafiki wakubwa sana.

Masengo alipofika Dar es Salaam alimchukua hadi Magomeni Maduka Sita nyumbani kwa Rais wa TANU Julius Nyerere kwenda kumtambulisha.

Screenshot_20221016-220324_Facebook.jpg
1665976809460.png
 
Back
Top Bottom