Nyerere Day 2025: Mwalimu Anastahili Sifa

Shalom mzee wangu Mohammed, wewe ni hadhina ya historia iliyotukuka ya taifa hili masikini
 
Kwenye post #2 Lupweko kashangaa kwamba kwa mara ya kwanza yeye jaona umemsema vizuri nyerere.. happhapo nawe ukamwambia akupe ushahidi kwa ww kumnanga Nyerere ndio ushahidi wa hiyo video ya dk17 hapo juu kakuwekea.
 
Kwenye post #2 Lupweko kashangaa kwamba kwa mara ya kwanza yeye jaona umemsema vizuri nyerere.. happhapo nawe ukamwambia akupe ushahidi kwa ww kumnanga Nyerere ndio ushahidi wa hiyo video ya dk17 hapo juu kakuwekea.
Inside...
Kurahisisha.

Hebu andika maneno unayoona yanamsema vibaya Nyerere.
Video hii ya. dak 17 naeleza historia ya Kura Tatu.

Nimeandika na kitabu kizima kuhusu Kura Tatu.
Hii ni historia muhimu sana.

Kura Tatu ndiyo iliyosababisha Zuberi Mtemvu kutoka TANU na kuunda Congress.

Kura Tatu ndiyo iliyoleta ugomvi baina ya Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU Sheikh Suleiman Takadir kugombana na Nyerere.

Kura Tatu ndiyo iliyosababisha Ramadhani Mashado Plantan na wanachama wengine kutoka TANU na kuunda All Muslims National Union (AMNUT).

Historia ya Kura Tatu niliyoandika mimi imeongeza elimu mpya katika historia ya uhuru wa Tanganyika.



Kushoto Sheikh Suleiman Takadir wa tatu Julius Nyerere na anaefuatia ni John Rupia


Kushoto John Rupia, Julus Nyerere na Zuberi Mtemvu
Nyuma waliosimama ni Bantu Group
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…