a4afrika
JF-Expert Member
- Apr 13, 2012
- 1,456
- 1,459
Tatizo lako ahali yangu ni kuwa unachambua sana KISIASA na sio KIUCHUMI.
Kumbuka umasikini wenu hauhusiani kabisa na SIASA ZENU bali ni UCHUMI WENU. Jaribu kupambanua alifanya nini kuhakikisha uchumi wenu unajengeka na kuwa stable?
Naomba nichangie kidogo...
Kuna kitu nahisi tumelishwa na kimejikita fikrani mwetu sisi watu weusi. Siasa, Uchumi na Utamaduni...kama nyanja kuu tatu za maisha ya binadamu!
Tumeaminishwa kwamba, mtu anaweza kuwa mwanauchumi na akawa si mwanasiasa au tamaduni. Yaani ni kusema kuwa Uchumi unaweza kusimama pekee pasi kuwa na Siasa na Utamaduni, au Siasa inaweza kujitegemea yenyewe pasi kuwa na Uchumi wala Utamaduni, vivyo hivyo kwa Utamaduni. Na matokeo ya imani hii ni kutokea kuzaliwa kwa mifumo KINZANI kuongoza njanja hizi tatu! Mfano mdogo leo, ni wazi kuwa HAKUNA muislamu safi kama anaamini katika Demokrasia, vile vile hakuna mkristo safi kama anaamini katika Ubepari, ni sawa na kumkuta mlokole ama jeshini! Leo hii tujiulize, nani hapa haishi Ubepari na Demokrasia? Je, Ukristo na Uislamu wetu tunauweka wapi? Haujafa tu? Je, Mifumo inayoongoza nyanja hzi tatu, INASHABIHIANA ama INAKINZANA? MATOKEO YAKE NI NINI KAMA SI KILA AINA YA UOVU NA UCHAFU TUUSHUHUDIAO LEO? Naita HESABU, zimetushika pabaya, only LOGIC to save us! Ni Mungu tu!
Binafsi naamini...
1. UCHUMI, has got nothing more than Physical and Biological Factors for Human Development.
2. SIASA. Ni mchakato wa kuratibu Uchumi. It is the procces!
3. UTAMADUNI. Ni jinsi/namna ya Uratibishaji wa Uchumi. The way is the the Procces! Mahusiano kati ya Uchumi na Siasa!
Kwa tafsiri hyo, mimi ni mwanasiasa, mwanauchumi na mwanatamaduni pia tangu kuzaliwa!
Labda tu nitamuita mtu mwanasiasa ama mwanauchumi au mwanatamaduni katika uwanja wa FASIHI tu. Kwani huko neno moja laweza beba lukuki ya maana!
*Nikirudi kwenye mada...
Kama alivyosema Mkuu wangu Nicholoas. Ni wazi kuwa mkono hauwezi kukataa kupaka dawa jeraha mguuni, kwani athari zake si kwa mguu tu, bali ni mwili mzima. Mafungamano yetu Afrika, ndiyo yaliyopaswa kutangulizwa kwanza! Huwezi kupona wewe mwanaafrika wa Tanzania, kama mkenya ana mafua. Uganda wakilia njaa, nasi tukakaa kimya, matokeo yake watatumia nguvu kuja kutuibia mifugo mpakani, hatutokubali tutapigana nao...ni VITA-MACHUNGU KOTEKOTE. Chanzo ni KUTOFIKIRIANA, OGOPA sana aina yoyote ya UMIMI, SISI KWANZA, kwani mwisho wake ni MAUMIVU. Ndicho KINACHOTUTOKEA LEO.
Viongozi weledi wachache wa Afrika Nyerere akiwemo, walishayaona haya mapema. HULKA na MATAMANIO yetu ambayo ndio mama wa UBINAFSI, ukapindisha UKWELI-MANTIKI-UTU. Leo tunalilia asali, halikuwa wenyewe tufuga manyigu na kuua nyuki.
Vijana siku hzi tunasema "TUNAONESHWA MATITI YA NYOKA"
HESABU KALI wanaafrika wenzangu. TUUMIZE VICHWA.
Mungu wetu anaita sasa!