Nyerere viwanda vingi alikuta vimeshajengwa na wakoloni

Nyerere viwanda vingi alikuta vimeshajengwa na wakoloni

Mpigania uhuru wa pili

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2023
Posts
3,380
Reaction score
6,376
Kumekua na upotoshaji mkubwa sana juu ya viwanda ambavyo vingi vilianza kufa miaka ya 1980's mpaka 2000's mwanzoni vikawa vimekufa vyote

Viwanda vingi sana hapa Tanzania vilijengwa na mkoloni ni vichache sana vilijengwa na nyerere na hata ukija kwenye miundombinu mingi kama reli nyingi zilijengwa na wakoloni

Moja ya sababu kubwa ya viwanda kufa ni kwa sababu sisi Tanzania hatukuvijenga bali tulirithi kutoka kwa wakoloni hatukujua uchungu na umuhimu wa kuviendesha

Viwanda vingi vilijengwa kwenye msingi wa ubepari ila baadaye vikawa vinaendeshwa kwa mfumo wa ujamaa changamoto ndo ilipo-anzia hapo mpaka vilipokufa
 
Sawa ila viko wapi?
1997 pale Moro ndio Polyster ilikuwa inamalizia uzalishaji wake Kama kiwanda cha ndani kabla hakijahamia huko Korea. Mwaka huo aliyekikuta alikuwa bado anakosimamia yeye?
Pale mbarali lipo shamba ambalo lilitengenezwa na mchina akaweka vifaa vyote humo 2006 likahamia kwa mwekezaji.
Hatukujenga ndio wala hayukutengeneza vikafa(kwa maelezo yako) Unajua hadi vinabinafsishwa vilikuwa bado vikifanya kazi? Vimekufa chini ya wawekezaji wala sio Watanzania
 
Mleta Uzi nmekuelewa kwamba sababu kuu ya viwanda kufa ni sisi watanzamia ambao hatukuvijenga na vipi kwa vile vichache tulivyojebga mbona pia vilikufa
 
Nyerere hayupo takribani miaka 25, viko wapi walivyojenga au kuendeleza hao waliofuata?
 
Tupe mifano ya viwanda vilivyojengwa na wakoloni.Vipo vingapi? Vilijengwa mikoa gani?
 
Mleta Uzi nmekuelewa kwamba sababu kuu ya viwanda kufa ni sisi watanzamia ambao hatukuvijenga na vipi kwa vile vichache tulivyojebga mbona pia vilikufa
Vile vya Magufuli na mwijage viko wapi?
 
kila zama na nabii wake, tusimlaumu JK. Nyerere yeye alishakwenda zake. vp viongozi waliopo hai wametufikisha wapi kuhusu viwanda?
 
Back
Top Bottom