Nyie mnaopenda kuiga biashara za watu hebu jaribuni kuweni wabunifu, mnaleta chuki ipo siku tutakuja kuonana wabaya

Nyie mnaopenda kuiga biashara za watu hebu jaribuni kuweni wabunifu, mnaleta chuki ipo siku tutakuja kuonana wabaya

Mohamedex121

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2022
Posts
1,725
Reaction score
3,271
Mbongo Aisee ni mtu mwenye kichwa kigumu sana. Imagine mtu unaona kabisa sehemu fulani kuna biashara kama nne zinazofanana we unaenda kuanzisha biashara hiyo hiyo, hivi hii inaingia akili kweli au mnataka watu tuanze kuitana wachawi??

Mtu unaona kabisa sehemu fulani kuna stationary na studio kama tano na wewe pia unataka unazishe stationary kisa tu umemuona fulani ana wateja wengi kwenye stationary na wewe umeamua kuleta biashara yako tuanze kugombania wateja mwisho wa siku watu tunaanza kuitana wachawi

Halafu isitoshe nyinyi mnaopangisha fremu utamruhusu vipi mtu afanye biashara the same kama wapangaji wengine wanafanya hiyo biashara, huko ni kuleta uchonganishi. Kugombanisha pasipo na sababu za msingi.

Hii kuigana igana biashara inatia hasira sana. Basi tu watu tunaamua kuishi hivo hivyo. Siku ya pili sasa wateja wamepungua sana ofisini kwangu. Itoshe kusema wabongo mnamauzi sana.
 
Mbongo Aisee ni mtu mwenye kichwa kigumu sana. Image mtu unaona kabisa sehemu fulani kuna biashara kama nne zinazofanana we unaenda kuanzisha biashara hiyo hiyo ivi hii inaingia akili kweli au mnataka watu tuanze kuitana wachawi??

Mtu unaona kabisa sehemu fulani kuna stationary na studio kama tano na wewe pia unataka unazishe stationary kisa tu umemuona fulani anawateja wengi kwenye stationary na wewe umeamua kuleta biashara yako tuanze kugombania wateja mwisho wa siku watu tunaanza kuitana wachawi

Halafu isitoshe nyinyi mnaopangisha fremu utamruhusu vipi mtu afanye biashara the same kama wapangaji wengine wanafanya hio biashara, huko ni kuleta uchonganishi. Kugombanisha pasipo na sababu za msingi.

Hii kuigana igana biashara inatia hasira sana. Basi tu watu tunaamua kuishi hivo hivo. Siku ya pili sasa wateja wamepungua sana ofisini kwangu. Itoshe kusema wabongo mnamauzi sana.
Kheeeeeeeeee..!! Unapajua Kariakoo..!!?? Unajuwa kuna maduka mangapi ya nguo? KWani una hati miliki ya biashara husika kwa sehemu husika?

AU nikuulize, Dar to Mbeya kuana mabasi mangapi? Kama wote wangekuwa na roho mbaya uliyonayo kwenye hili, ingekuwaje kwenye hiyo biashara ya mabasi?

Wewe kule sokoni unakokwenda au unakotuma watu waende kununua nyanya, kuna wangapi wanafanya biashara ya nyanya..??

Hata mkiwa wengi kwenye eneo moja na biashara moja, fuata zile P nne ili uwashinde wenzio;
1. Place
2. Price
3. Product
4. Packaging

Mwanamke nyonga kwenye bia ilishawahi hamisha watu kutoka bia moja kwenda nyingine.
 
Mbongo Aisee ni mtu mwenye kichwa kigumu sana. Imagine mtu unaona kabisa sehemu fulani kuna biashara kama nne zinazofanana we unaenda kuanzisha biashara hiyo hiyo, hivi hii inaingia akili kweli au mnataka watu tuanze kuitana wachawi??

Mtu unaona kabisa sehemu fulani kuna stationary na studio kama tano na wewe pia unataka unazishe stationary kisa tu umemuona fulani ana wateja wengi kwenye stationary na wewe umeamua kuleta biashara yako tuanze kugombania wateja mwisho wa siku watu tunaanza kuitana wachawi

Halafu isitoshe nyinyi mnaopangisha fremu utamruhusu vipi mtu afanye biashara the same kama wapangaji wengine wanafanya hiyo biashara, huko ni kuleta uchonganishi. Kugombanisha pasipo na sababu za msingi.

Hii kuigana igana biashara inatia hasira sana. Basi tu watu tunaamua kuishi hivo hivyo. Siku ya pili sasa wateja wamepungua sana ofisini kwangu. Itoshe kusema wabongo mnamauzi sana.
Bidhara bongo ngumu Sana.
 
Pole sana utawalaumu bure hao watu lakini hayo ni matokeo ya mfumo wa elimu na malezi kwa ujumla.
Elimu imefifisha ubunifu na inazidi kuumaliza kabisa, hatuwezi kushughulika na matawi wakati mizizi imejikita chini
Aisee acha tu mkuu watu hawawazi kuwa wabunifu ni kuigana igana tu. Acha tu tuishi nao hivo hivo
 
Aisee acha tu mkuu watu hawawazi kuwa wabunifu ni kuigana igana tu. Acha tu tuishi nao hivo hivo

Watu hawana exposure toka wamezaliwa wanatoka dar kwenda iringa, mbeya, morogoro mwanza.
Mabando yamepanda bei sasa watajifunza kutoka wapi kama sio kuiga tu.

Tugawane riziki hivyo hivyo mkuu hakuna namna
 
Acha zako, kila mtu na riziki yake....kama ni hivyo Kariakoo ifungwe....wewe ni mbinafsi
Kwani location zingine huzioni mpaka un'gan'ganie sehemu ambayo watu umetukuta tunafanya biashara the same ambayo wewe unayotaka kufanya. Nyie ndio mnaoleta chuki na ushirikina. Why usitafute location nyingine
 
Watu hawana exposure toka wamezaliwa wanatoka dar kwenda iringa, mbeya, morogoro mwanza.
Mabando yamepanda bei sasa watajifunza kutoka wapi kama sio kuiga tu.

Tugawane riziki hivyo hivyo mkuu hakuna namna
Aisee mimi siwezi hili suala la kugawana ni bora nihame nitafute location nyingine
 
Wafanyabiashara wanapokuwa wengi sehemu flani tunaonufaika ni wateja kwasababu ya ushindani hasa kwa mapunguzo ya bei, na hii ni sababu mara nyingi wafanyabiahara wa eneo hilo hawana umoja kila mtu anatumia mbinu zake kupora wateja wa wenzake.

Hofu yetu wateja huwa ipo wafanyabiashara wanapoungana, furaha yetu wateja ipo wafanyabiashara wakikosa umoja, kuchukiana, kuzungukana, n.k.
 
Back
Top Bottom