Nyie mnaopenda kuiga biashara za watu hebu jaribuni kuweni wabunifu, mnaleta chuki ipo siku tutakuja kuonana wabaya

Nyie mnaopenda kuiga biashara za watu hebu jaribuni kuweni wabunifu, mnaleta chuki ipo siku tutakuja kuonana wabaya

Kheeeeeeeeee..!! Unapajua Kariakoo..!!?? Unajuwa kuna maduka mangapi ya nguo? KWani una hati miliki ya biashara husika kwa sehemu husika?

AU nikuulize, Dar to Mbeya kuana mabasi mangapi? Kama wote wangekuwa na roho mbaya uliyonayo kwenye hili, ingekuwaje kwenye hiyo biashara ya mabasi?

Wewe kule sokoni unakokwenda au unakotuma watu waende kununua nyanya, kuna wangapi wanafanya biashara ya nyanya..??

Hata mkiwa wengi kwenye eneo moja na biashara moja, fuata zile P nne ili uwashinde wenzio;
1. Place
2. Price
3. Product
4. Packaging

Mwanamke nyonga kwenye bia ilishawahi hamisha watu kutoka bia moja kwenda nyingine.
Ongezea 5: customer care

Naona mkubwa ana makasiriko 🤓
 
Usiwezi kupoteza huo muda wakati umeleta mtu anayefanya biashara ninayoifanya mimi kama ulimpa mkataba wa pango basi rudisha kodi hakukuwa na haja ya kunipangisha zaidi ya kuleta uchonganishi
Nimejenga frem Kwa ajili ya biashara hata kama frem zangu 10 wote watafanya biashara Aina moja Mie hainihusu cha msingi fremu zangu hazidoda
 
Ujamaa umeharibu akili za wabongo wengi, hapo ulipo wewe mpo wanne je mlianza pamoja? Je nyie watatu mlioyemkuta wa Kwanza je mlisababisha ashindwe kupata wateja?
Kuongezeka kwa biashara ya aina moja sehemu moja INAPUNGUZA MAUZO NA WATEJA kwa wale waliotangulia wengine usipokomaa unaishia kufungaa. hapo ndo uchawi huanza
 
Kwa k'koo hata mkifanana sio tabu,kila mtu na wateja wake na maisha yanasonga

Ila Kuna mahali pengine nmepanga,

Mwenye fremu nae anauza pale pale, Ila sharti lake uziuze bidhaa anayouza yeye au mwenzako.

Pia hapangishi fremu 2 wote muuze bidhaa za aina moja

Hoja zake ndo hizo za kugombaia wateja nakurogana[emoji4]
 
Mbongo Aisee ni mtu mwenye kichwa kigumu sana. Imagine mtu unaona kabisa sehemu fulani kuna biashara kama nne zinazofanana we unaenda kuanzisha biashara hiyo hiyo, hivi hii inaingia akili kweli au mnataka watu tuanze kuitana wachawi??

Mtu unaona kabisa sehemu fulani kuna stationary na studio kama tano na wewe pia unataka unazishe stationary kisa tu umemuona fulani ana wateja wengi kwenye stationary na wewe umeamua kuleta biashara yako tuanze kugombania wateja mwisho wa siku watu tunaanza kuitana wachawi

Halafu isitoshe nyinyi mnaopangisha fremu utamruhusu vipi mtu afanye biashara the same kama wapangaji wengine wanafanya hiyo biashara, huko ni kuleta uchonganishi. Kugombanisha pasipo na sababu za msingi.

Hii kuigana igana biashara inatia hasira sana. Basi tu watu tunaamua kuishi hivo hivyo. Siku ya pili sasa wateja wamepungua sana ofisini kwangu. Itoshe kusema wabongo mnamauzi sana.
Usiwe na wasiwasi huo kwenye biashara, hilo ni dunia nzima na ndipo biashara yako uliyeanzisha inakuwa na uhai mzuri.

Kinachotakiwa, kama ulivyisema, kuxidisha ubinifu. Unatakiwa wewe hapo uzidishe ubunifu kwenye biashara yako.

Ukitembea duniani kwenye ma biashara (hata Kariakoo) utakuta mtaa mzima au mitaa miwili mitatu inafanya biashara zinazolinga. tofauti ni ubunifu waa kila mmoja. Kama ni spae za magari utakuta maduka yote pamoja.

Saikolojia ya wanunuzi ni kutokwenda ambako ipo biashara hiyo moja peke yake. Akikosa kwako anachohitaji aondoke aende mji mwengine? Au aende upande wa pili wa mji? Utazowe tu biasara, biashara ni kazi ngumu na inayohitaji uzoefu. hata ukiendaa vibanda vya pombe utakuta watu wanaenda vilabuni ambako wauzaji ni wengi na tofauti. Hata madanguro utakuta yamegjazana au wauza miili wamejazana.

Biashara za "exclusivity" zina namna zake, labda ueleze ni biashara ipi tukupe mbinu upige mabao.
 
Kuongezeka kwa biashara ya aina moja sehemu moja INAPUNGUZA MAUZO NA WATEJA kwa wale waliotangulia wengine usipokomaa unaishia kufungaa. hapo ndo uchawi huanza
Upo sahihi kabisa, mwisho wa siku mnaanza kuitana wachawi wakati kosa ni dogo kwanini asitafute sehemu nyingine afungue stationary yake
 
Kuongezeka kwa biashara ya aina moja sehemu moja INAPUNGUZA MAUZO NA WATEJA kwa wale waliotangulia wengine usipokomaa unaishia kufungaa. hapo ndo uchawi huanza
Biashara ya kuigana Kariakoo tu ndiyo Imefanikiwa...

Imagine unakuta mtaa mmoja wote Biashara ni moja...Mtaa mwingine hivyo hivyo..
Na kila Duka linauza..
 
Kuongezeka kwa biashara ya aina moja sehemu moja INAPUNGUZA MAUZO NA WATEJA kwa wale waliotangulia wengine usipokomaa unaishia kufungaa. hapo ndo uchawi huanza
Ndo soko huria lilivyo na sio dhambi kuiga biashara wala Sheria haijavunjwa so imagine we uzuiliwe kufanya biashara ambayo tayari inafanywa na wengine nazani unaweza kwenda kujitoa mhanga ikulu, sifa kuu ya soko huria ni ushindani na ktk ushindani tunapata vitu Bora na fanisi so heri Kwa sie consumer tunakuwa wigo mpana wa kuchagua anayetoa huduma Bora.
 
Back
Top Bottom