James Hadley Chase
JF-Expert Member
- Mar 25, 2020
- 1,984
- 3,695
WAKATI nakua na kupata fahamu za kujua kuwapo kwa Mungu, ipo siku wazazi wangu waliniamsha alfajiri na kunivisha nguo ambazo sikuwahi kuzivaa, zilikuwa mpya; shati na kaptura, tofauti na zamani nikivaa shati refu tu bila kingine chini.
Baada ya kuvishwa nguo hizo nikiwa nimemaliza kuoga, tukala kiporo na kisha kuambiwa tunakwenda mahali nisikokujua na wala nisikotakiwa kuhoji. Safari ilikuwa ndefu kidogo ya mguu, mara nikibebwa na wakati mwingine nikitembea.
Kumbuka sikuwa nimeanza shule, nilikuwa bado kijamaa fulani kidogo hivi nikinyolewa nywele kwa mkasi, kinyozi baba yangu.
Baada ya safari Kidogo, tukafika jengo fulani refu na kubwa kuliko nyumba tuliyokuwa tukiishi; ya udongo na nyasi.
Tulipoingia ndani, nikasikia nyimbo kila mtu aliyekuwa ndani akiimba.
Tukakaa mahali hivi na wazazi wangu ndipo mtu mmoja akiwa mbele akawa anatuongoza tukisimama na kuimba na mara nyingine kupiga magoti.
Sikuwa najua lolote lililokuwa likiendelea, bali kufuatisha walichofanya wazazi wangu na watu wengine waliojaa mjengoni ambamo baadaye nilikuja kuambiwa linaitwa kanisa na tulikuwa tukienda hapo kila Jumamosi kumwomba Mungu.
Ufahamu na utambuzi ulipozidi kuongezeka, nikataka kumjua huyo niliyekuwa namsikia akitajwa mara zote kwa jina la Mungu. Hatimaye, nikaambiwa ndiye aliyetuumba sote sisi binadamu, lakini siku zote yeye hafiki kanisani bali anaishi mbinguni.
Nikataka kujua mbinguni ni kijiji au mji gani. Nikaambiwa ni huko juu ndiko anakoishi akitufuatilia sisi tulioko huku duniani. Picha ikawa inanijia hasa nilipokuwa nikisikia maneno kama ya aliyeko huko juu mbinguni, ingawa mara nyingi nikitazama juu niliishia kuona mawingu.
Ilinipa matumiani makubwa pale mvua iliponyesha, nikisika wazee wakimshukuru Mungu kwa kuwaletea mvua. Kumbe walikuwa wakishukuru, kwa sababu bila mvua hakuna mazao. Ndipo nikaamini kuwa kumbe huyo Mungu ana uwezo mkubwa.
Nilipoamini hivyo, nikapewa ‘madini’ mengine tena kuwa Mungu huyo ndiye mmiliki wa jua pia upepo, kwamba akiamua leo jua lisiwake haliwaki au upepo ukatike unakatika.
Alitumiliki sote kama baba alivyomiliki mifugo. Baadaye nikakua na kuelewa kila kitu, nikajua hata kuomba mwenyewe, nikaenda kanisani mwenyewe, nikiambiwa kuna siku Mtoto wa Mungu anayeitwa Yesu naye atakuja kutusalimia na kutuchukua twende naye kumwona Mungu mbinguni.
Furaha iliyoje!
Enzi hizo nakumbuka kuwapo makanisa machache na misikiti, yote yakiwa majengo ya ibada, ya kumwabudia Mungu, kumwomba na kumshukuru kwa alichotupa hata kama tulilima wenyewe, lakini tukimshukuru kwa kutupa nguvu za kulima.
Nikawa nasikia Kanisa Katoliki, Kanisa la Sabato, Kanisa Anglikana, Kanisa la Pentekoste na Kanisa la Menonaiti na misikiti, basi. Hayo tu, na tukigawanyika hawa wakienda kule Ijumaa, wengine Jumamosi na wengine Jumapili, lakini wote kumwomba Mungu mmoja.
He! Ghafla sijui ukaibuka upepo gani, yakaja mengine kama utitiri, nikiyataja hapa nitamaliza ukurasa! Haya sasa yakawa hayana hata siku maalumu, yanaibukia kokote kuendesha ibada na tena siku yoyote!
Haya sasa yanachangisha fedha za watu kwa jina la Fulani, kwa kiwango kikubwa tofauti na awali tukitoa sadaka kwa hiari, lakini haya ya sasa ni lazima na yakiona mbishi yanakuja na vitisho vya usipotoa hupati baraka za Mungu!
Utalazimika kununua bidhaa zao kwa bei waitakayo wakikwambia ukifanya hivyo ndipo utafanikiwa katika maisha yako.
Watu wanaibiana mali kwenye ndoa wanapelekea ili kupata uzima, watu wanajinyima kula wakiacha kununua chakula cha familia wanawapelekea.
Yametokea nchi jirani, watu kwa mamia wamekufa kwa imani tete kama hizo. Sasa, bila kutoa risiti, tunakaba wafanyabiashara huku hawa tukiwaacha, Kwanini? Hivi TRA mnafanya nini?