Nyie wadada, tupatieni namba zenu za simu

Nyie wadada, tupatieni namba zenu za simu

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Wengi katika mahusiano, huanza kwa kupeana namba za simu, na baadaye kuanza kuwasiliana, na hatimaye kuelewana katika mahusiano wanayotaka kuyaanzisha.

Wakati mwingine kupewa namba ya simu imekuwa changamoto; unaweza ukaomba, na ukaishia kuzungushwa tu, na baadaye kutokuendelea kumsumbua muhusika.

Kwa asilimia kubwa, sisi wanaume ndio tunao ongoza kwa kuomba namba za simu, pale unapokuwa umevutiwa na mwanadada aliyeteka moyo wako.

Tatizo linakuja pale, kwenye kupewa namba ya simu; unaweza ukazungushwa kama unasaka ajira vile.

Atataka ajue uwezo wa kipato chako, umaarufu wako n.k, na kama ataona huna hivyo vigezo, unaishia kudharauliwa tu.

Nyie wadada, kwanini mnatuzungusha sisi wanaume hivyo? Hamjui, bila kuwa na mwanaume; unakuwa haujakamilika?

Naishia kusema, tupeni namba zenu za simu bila masharti yoyote.​
 
Huu utongozaji wa siku hizi ni changamoto. Enzi zile watu hawakuwa na simu, walikuwa wanatongozana uso kwa uso. Huo muda unaotumia kuomba namba ya simu nadhani ndo ungeutumia kumtongoza huyo mrembo aliyekuvutia
Teknolojia imerahisisha mambo
 
Wewe mzee baba unawajukuu unataka nini tena jamani siukae nyumbani sasa hivi ndoto unazotakiwa uote ni za mbinguni tu mrejee Mungu wewe umezeeka 55 sio mchezo eti unajitahidi sana kwa tozo hizi na kile kiduka aisee hongera sana big up hujapatwa na presha.
Maisha ya hapa duniani ni matamu sana; na hakuna maisha mengine zaidi ya haya. Mambo ya mbinguni tunadanganyana.
 
Hupatiwi namba because umri umesogea watu wanaogopa kukupa namba wasiwe wakawa israeli huko gesti bila kukusudia
Msitufanyie hivyo, hivyo ni kututenga sisi; kumbuka nasi tunahisia kama binadamu wengine.
 
Back
Top Bottom