Nyie wauza maziwa kwa nini mnaweka maji

Nyie wauza maziwa kwa nini mnaweka maji

BABA SANIAH

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2013
Posts
4,606
Reaction score
5,922
aisee nyie wauza maziwa mnazingua sana,sometime mtu umeamua kwenda kupata maziwa ili uboreshe afya unakuta mmejaza maji mpaka ladha inapotea.ndo vyuma vimekaza au,na sisi wanywaji ia mambo si mambo atii
mmasai aliekamua kwa mifugo yake kaweka maji
wewe shekimweri nawe unaweka maji
mteja akinywa paleale yanakuwa yameshawekwa maji
mteja akipeleka home kaamua siku hiyo na familia iige tea ziwa nae anaweka maji,kwa kuwa familia basi yatoshe,
angalia sasa
masai kaweka maji baada ya kukamua
shekimweri nae kanunua kwa masai anatuuzia kwenye kibanda kaweka maji
baba jamillah nae kanunua kwa shekimweri iili kina jamillah wakanywe tea ziwa anampa mama jamillah nae anaweka maji,sasa tunakunywa maziwa au harufu na rangi ya maziwa.
acheni hizo aisee mnatuzingua kwa sana
 
Wanaweka maji ili yawe mengi.

Mimi kuna siku nilinunua maziwa, nilitaka mtindi nikakosa, nikapata fresh. Si nikakulia limau ili yagande? hayakuganda, nikazidi kuongeza limau ili yagande, Cha ajabu hayakuganda bali yalibadili ladha yakawa machachu kama limau, ndipo nilipogundua hayakuwa maziwa bali maji yene rangi ya maziwa.
 
Ni ushenzi tuu na tamaa,ninafuga lakini sijawahi kuweka maji au kuuza maziwa ya ngombe mgonjwa,au anayetibiwa,ungekuwa karibu ningekukaribisha uonje maziwa halisi ya ngombe,.....
 
Mkuu hili linatokana na mfugaji kuwa nawa teja wengi hivyo anajikuta maziwa ya kuwapa hana anaamua kutia maji ili yaongezeke apate pesa, ila kuna wafugaji wengine ni waa minifu hawatii maji kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mshikaji ilikuwa ukienda kwake anakukamulia kwenye dumu unamuona,watu tukasema hatii maji ni freshi kabisa akapata wateja wengi sana.

Siri ikavuja kwaamba kumbe huwa anatanguliza maji kwenye dumu anayaweka then akikamua maziwa mule ndani yanakutana na maji ya kitambo kileer.

Ila waswahili tunashida sana.

Mtu atataka maziwa yasiyotiwa maji alafu kwake anaenda kuzimua ili wapate vikombe vitano vya kunywa familia nzima.
Hahahaha
 
Mkuu hili linatokana na mfugaji kuwa nawa teja wengi hivyo anajikuta maziwa ya kuwapa hana anaamua kutia maji ili yaongezeke apate pesa, ila kuna wafugaji wengine ni waa minifu hawatii maji kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli mkuu kuna dada alikuwa ananiuzia maziwa fresh yaani mazito baadae alipo Pata wateja wengi aisee anaweka maji kwa Sasa nimestop kununua kwake
 
Back
Top Bottom