Nyie wazazi msitupangie matumizi ya pesa

Nyie wazazi msitupangie matumizi ya pesa

Mwizukulu mgikuru

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2021
Posts
6,788
Reaction score
16,227
Jana kwenye harakati zangu nikawa nimepata viji laki kadhaa. sasa miaka ya nyuma kuna binti nilipata kuzaa nae (waislamu wanaita mtoto wa haramu) nimekuwa nikipambana sana kupata taarifa za yule mtoto kuhusu maisha yake na afya yake pia , kuna nyakati nilikuwa nanunua nguo na vitu vingine kwa matumizi ya mtoto navituma huko mkoa x alipo mtoto.

Lakini kama mnavyofahamu wanawake wengi wa kileo (gen z) nilikuwa naambulia matusi tu. yaani nilikuwa nashurutishwa nitume pesa badala ya vitu...sasa Mungu si athumani yule mwanamke kapata jamaa na kaolewa na yule mtoto akamtelekeza kwa ndugu zake.

Nikaona huu ndio muda muhimu wa kufurahia na damu yangu..yule mtoto ni wa kiume na ananifanana kwa kila kitu, nikachukua kama laki tatu hivi nikaingia sokoni nikanunua nguo, viatu na vitu vingine muhimu vya mtoto..nikafika maeneo alipo mtoto nikamuona nikafurahi sana na mtoto alipoambiwa huyu ni baba yako akashangilia kweli..

Nikachukua kumbukumbu ya picha ili nimuonyeshe mzazi wangu anaeishi mkoa x , nikamuhadithia kila kitu nikijua nae atafurahi kama mimi, eti anauliza kwanini laki tatu yote kwa matumizi ya mtoto, nimemjibu pesa natafuta mwenyewe na ukizingatia kwenye historia ya maisha yangu hajawahi kuchangia chochote labda maombi ya mzazi kwa mwanae...HAWA WAZAZI WASITUPANGIE MATUMIZI YA PESA ZETU.
 
Jana kwenye harakati zangu nikawa nimepata viji laki kadhaa. sasa miaka ya nyuma kuna binti nilipata kuzaa nae (waislamu wanaita mtoto wa haramu) nimekuwa nikipambana sana kupata taarifa za yule mtoto kuhusu maisha yake na afya yake pia , kuna nyakati nilikuwa nanunua nguo na vitu vingine kwa matumizi ya mtoto navituma huko mkoa x alipo mtoto lakini kama mnavyofahamu wanawake wengi wa kileo (gen z) nilikuwa naambulia matusi tu. yaani nilikuwa nashurutishwa nitume pesa badala ya vitu...sasa mungu si athumani yule mwanamke kapata jamaa na kaolewa na yule mtoto akamtelekeza kwa ndugu zake , nikaona huu ndio muda muhimu wa kufurahia na damu yangu..yule mtoto ni wa kiume na ananifanana kwa kila kitu, nikachukua kama laki tatu hivi nikaingia sokoni nikanunua nguo, viatu na vitu vingine muhimu vya mtoto..nikafika maeneo alipo mtoto nikamuona nikafurahi sana na mtoto alipoambiwa huyu ni baba yako akashangilia kweli..nikachukua kumbukumbu ya picha ili nimuonyeshe mzazi wangu anaeishi mkoa x , nikamuhadithia kila kitu nikijua nae atafurahi kama mimi, eti anauliza kwanini laki tatu yote kwa matumizi ya mtoto, nimemjibu pesa natafuta mwenyewe na ukizingatia kwenye historia ya maisha yangu hajawahi kuchangia chochote labda maombi ya mzazi kwa mwanae...HAWA WAZAZI WASITUPANGIE MATUMIZI YA PESA ZETU.
Wazaz wako wana roho mbaya tu. Sasa laki tatu si umehudumia mwanao, ye inamuuma duh.
 
Back
Top Bottom