Syston
JF-Expert Member
- Nov 6, 2017
- 243
- 351
Mnamo karne ya uwepo wa Mrusi hapa nchini, wakati huo Hayati baba wa taifa,Mwl. JK Nyerere alipomruhusu Mrusi awekeze katika ujenzi wa bwawa la kufua umeme katika eneo la Kijungu, maarufu kama DARAJA LA MUNGU, huko Mbeya.
Katika uchunguzi wa awali wa eneo hilo Urusi iligundua kuwa eneo lile lina madini aina ya MERCURY, kulingana na jiografia ya zamani ya Tanzania ilikuwa ni ngumu kwa maeneo yote kufikika kirahisi, Kwa kutumia Mwanya huo mrusi aliacha kazi iliyomleta na akaanza kuchimba madini hayo.
Ishu sasa ikaja kuyavusha ng'ambo kwani palikuwa na mto wa asili ambao uliweza kuvukika kwa kutumia Daraja la Mungu. Warusi walipojaribu kuvuka daraja hili wakiwa na madini nyoka huyu aliwazuia na alikuwa mkali mno.
Wakaamua kujenga daraja upande wa pili na wakaanza kusafirisha madini hayo kwa siri wakitoroshea kwao.
Nyerere alipoona mda umepita bila taarifa yoyote kutoka kwa watu hawa akaamua kwenda lakini alipofika daraja la mungu nyoka yule alimzuia kuvuka, ikabidi atume wasaidizi wake wakaangalie kunaendeleaje huko ng'ambo.
Walitahamaki kukuta daraja limejengwa na ajabu ni kuwa daraja hilo liliishia katika nyumba walipoishi Warusi na hakukuwa na njia inayoendelea Zaidi.
Baada ya taarifa hiyo Nyere aliamuru Warusi waondoke mara moja na kwa sababu hawakuweza tena kubeba madini waliamua kuyaficha kwa kudai wanaweka alama za ardhi(beacon), Nyerere akaamrisha askari waishi nyumba zile na iwepo kambi eneo lile.
Miaka kadhaa baadae Warusi walirud kufuata madini yao lakini walistaajabu walipokuta kuna kambi ya askari hivyo wakarudia mbali.