Nyifwila, nyoka aliyemzuia mwl. JK Nyerere kuvuka daraja la Mungu

Porojo za kizamani tu
Hakuna cha Nyifwila wala chochote
 
Mara ya mwisho kumwona ni 2009 ,alimulika nusu saa katka safu za livingstone mounts, mzee mmoja akaniambia kesho usiondoke kuna msiba,maana nilipanga kusafiri,nikaamuuliza why akasema hujamwona yule nyoka?

Asubuhi babu mmoja kafariki kweli,nilishangaa sana
 
KashAbalehe ndio maAnA uMUoni>....
 
Hivi hamna historia ya maana km vile hao mashujaa wenu kuwapiga nchi nyingine?Au hao wanaojiita mashujaa wa usalama wa taifa na majeshi ya kupiga raia,tusikie waliweza hamisha mahela nchi fulani, wakashinda kesi kadhaa za kiuchumi?
 
Hizi Mali za mzungu navyo wajua wabongo wangekuwa washavuta mpunga kitambo sana
 
Madini yapo ila ni eneo lenye maajabu mpaka kupita tu pale kuna masharti ya kimila. Pia kama ujuavyo kuna mali nyingi za mkoloni maeneo ya Tanzania ila zimehifadhiwa kimila so ukienda macho kumchuzi ndio mwisho wako.
Wewe unachanganya kijungu na daraja la mungu, kijungu ndio huwezi kuvuka ila daraja la mungu unapita tu bila wasiwasi, nimepita sana kwenye lile daraja hamna kitu niliona.
 
Mkuu, Mafuta yake yalikuwa yakionekana kwani?
 
Ningependa kujua zaidi kuhusu huyu nyoka
Wenye habari zake watuambie kama bado wapo
Nyoka anawasha taa duh😳😳😳
 
Kuambiwa ndio kumwona ?

Halafu hizi ni imani tu hazina uhalisia
 
Nilishawahi kumsikia huyu Nyifwila kama nyoka mwenye vichwa vingi. Wenzetu wanaita dragon. Jamii nyingi sana zina aina hii ya viumbe (fikirika), hata nchi za magharibi. Uskoti (Scotland) wana Neiss wa Loch Ness ambaye wamemfanya kivutio cha utalii. Huko Norway wana kiumbe aliyetambulika kama Kraken, aliyeaminika kuwinda wavuvi. Sasa hivi ni chapa inayojulikana na kutumika kwenye filamu, vitabu, vinywaji, nk.

Hata huyu Nyifwila ni jinsi tu tukavyoamua kumchukulia. Anaweza kuwa sehemu ya kivutio cha utalii wa Daraja la Mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…