Nyimbo maarufu kwenye maharusi na shughuli mbalimbali

Nyimbo maarufu kwenye maharusi na shughuli mbalimbali

Kuna nyimbo ambazo binafsi nikienda kwenye sherehe mbalimbali haswaa harusi ni nadra kuzikosa, hii inatokana pengine na kukubalika na wengi, na hii inaweza kuwa ni njia nzuri ya msanii kujifanyia research nyimbo zake zinapokelewa vipi mtaani, wimbo unaweza ukawa haupewi sana promo kwenye redio ila kitaa raia wanauelewa, hizi ni baadhi;

1. Ole Themba-Lina (Hii imekimbiza sana kuanzia mwakajuzi, kila kasherehe ni ngumu kuikosa, ingawa kwa sasa imechuja kidogo

2. Duro - Tekno (Ukiacha Duro huyu jamaa nyimbo zake karibu zote ni 'hit' kwenye maharusi, yaani ni ngumu kuona harusi nzima haina hata wimbo mmoja wa Tekno iwe Duro, Wash, Where, Diana, sijajua kwanini nyimbo zake zinapendwa sana kwenye matukio)

3. Nani Kama Mama -Bella & Dimpoz (huu wimbo ni ngumu sana kuukosa hasa kwenye kipengele cha Mama mzazi wa bw/bibi harusi)

4. Huyo ni chaguo lako - Manesa Sanga (Huu wimbo ni ngumu kuukosa)
5. Ni kwa neema tu - Edson Mwasabwite (Huu nao haukosekanagi)

6. Nana & Number One - Diamond (Hizi ni nyimbo zilizohit sana kwenye maharusi ingawa naona kwa sasa hazichezwi sana, ingizo jipya la Diamond ni Salome, nao naona unajitutumua katika nyimbo zinazopendwa kwenye maharusi)

7. Wimbo wa Kanda Bongoman (Nimeusahau jina)
8. Ekotite - Koffi Olomide (Nadhani kila anayehudhuria maharusi hawezi kubisha kuhusu huu wimbo)

9. Nagode Remix - Yemi Alade (Huu wimbo umekimbiza sana mwakajana, na mwakahuu bado umo)
10. Taarabu za mzee Yusuph na Kwaito - (hivi vitu ni ngumu sana kukosekana)
11. Jah Prayzah ft Diamond - Watora Mari (huu wimbo hauchezwi sana redioni lakini karibu kila sherehe niliyohudhuria miezi ya hivi karibuni nimekuwa nikikutana nao na watu wanauelewa sana)
12...........
13.....

NB: Haka ni kautafiti ka huku mkoani kwetu, sijui kwenu huko wanaume wa dar
list yako haija kamilika kama nyimbo ya

BoB Ludala ya Nime kuchagua wewe

eti haipo???
 
Naomba uniamini > Jose Chammelion
 
kuna carolina (sijui kaimba nani ila ni mkongo nahisi) na Moja Ya extra musica .........watu wa rika langu na la nyuma kidogo huwa wanayarudi sana
 
Kwenye hiyo list ongeza Tupogo kutoka timu mziki mzuri a.k.a wakupumuliwa
 
Ndoa by joseph nyuki...zunguka by enock...dada remmy rmx by remy ongala....safari by juma kekere...dodo by davido....msishangae sana ni ni Dj nafanya hzo kazi
 
Back
Top Bottom