Nyimbo ''Madhulumu Moyo'' na Historia ya Kwa Bamkwe 1972

Nyimbo ''Madhulumu Moyo'' na Historia ya Kwa Bamkwe 1972

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
NYIMBO MOYO MADHULUMU NA HISTORIA YA KWA BAMKWE
Siku ya kwanza alipouimba mwimbo huu "Moyo Madhulumu," hadharani marehemu Khadija Baramia hakuweza kumaliza katikati alianza kulia na hakuweza kunyamaza.

Wasikilizaji wanawake nao wakalia.

Ikhwan Safaa wapigaji orchestra iliendelea kupiga ala kwa muda vyombo vikipigwa wakiamini muimbaji ataimba.

Khadija Baramia hakuweza kurejea kwenye hali yake kwani majonzi ya kuuliwa mumewe machungu yake yalimrudia upya.

Ikhwan Safaa ikazima ala zote.
Pakawa kimya.

Hali kama hii haikupata kutokea.

Toka mahojiano yangu na Mohammed Ghassani yatoke nimekuwa nikipokea msg nyingi na najitahidi kujibu kushukuru kwa wasikilizaji kuonyesha hisia zao.

Hivi niandikapo watu walioangalia video hii wamefika 6000+ na wanaendelea kuingia.

Wanaoniandikia na wengine kunipigia simu wanasema Bamkwe haijesha bado ipo nk. nk.

Mohammed Ghassani kalisema hili katika mazungumzo yetu.

Mohammed Ghassani anasema, "Ubamkwe" na "Umandera" bado uko Zanzibar.

Mbele yangu nina kitabu, "Mauaji ya Kutisha ya Elfu Mbili na Moja."

Kitabu hiki alinipa Prof. Ibrahim Haruna Lipumba na aliniandikia maneno haya na kutia saini yake katika jalada ndani ya kitabu:

"Dear Mohamed,
Please critically read this book and please make an effort to write your own account by interviewing survivors of the massacre.

I believe you will write even a better and vivid account."

Hili sikulifanya.
Wakati ule ilikuwa mapema mno.

Utafiti kama huu unataka kupewa muda vidonda na machungu yapone.
Wajane wapite ile hali ya upweke na kuomboleza.

Watoto wawe wamepata umri na kuwa faraja kwa mama zao.

Nimefika Pemba 2023 baada ya miaka 22 toka yatokee mauaji yale baada ya uchaguzi wa 2000.

Nimetembea kwingi, nimeona mengi, nimesikia mengi na nimejifunza mengi.

Uchaguzi wa 2020 Wazanzibari 21 wameuliwa.
Huu ni ushahidi kuwa Zanzibar bado inayo Mandera wa zama zetu?

Kepteni Meki mumewe Khadija Baramia alipigwa risasi na Abdallah Kaujore wakati akikagua watuhumiwa waliotiwa mbaroni baada kuawa Mzee Karume.

Wakati anampiga risasi Kaujore inasemekana alisema maneno haya, "Huyu angeniua miye kwanza ngoja nimuwahi...."

Haya kaniandikia msomaji wangu.
Nimepokea mengi ya zamani na ya hivi karibuni.

Sikutegemea kabisa kama kitabu cha Ibrahim Hussein Mohammed, "Baraza ya Majestic na Machinjioni Kwa Bwamkwe," kitaibua katika jamii ya Wazanzibari hisia kali na kurejesha kumbukumbu za historia mbaya iliyoikumba Zanzibar baada ya mapinduzi.

1724161827775.jpeg
 
Kuzungumzia mambo ya nchi ya Zanzibar ni kupoteza muda.

Tuna mambo mengi ya kuzungumza kuhusu nchi yetu ya Tanganyika
 
Mna...
Hitler na Gestapo waliua Wayahudi wengi sana.

Je hawa Wayahudi waliouawa Auschwitz na kwengineko walikuwa, "wapuuzi?"
Ndio wayahudi walikuwa wapuuzi au umesahau kuwa hata Quran imeeleza hivyo kuhusu wayahudi?
 
Back
Top Bottom