Nyimbo tulizoimba tukiwa shuleni

kidaganda

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2013
Posts
2,995
Reaction score
2,572
Tujikumbushe nyimbo tulizowahi imba tukiwa shule za msingi darasani au kipindi cha mchaka mchaka....



sina nguvu tena eenhe
ya kuua simba eenhe
simba ni mkali eenhee
aliua kuku eheee
akaua fisi eenhee


[emoji23][emoji23]haya wahi wahiii


eenheeeeeee
 
Nyie watu mna miroho kama ya paka hata ham comment ila ingekuwa post ya kina fidodido hata kama utumbo mngesapoti.
 
Baba na mama wee nipelekeni shulee
Na mimi nikajueee
Kusoma na kuandikaa.
Wenzangu wanajuaaa
Kusoma na kuandika mimi nahangaika kama mpita njiaa. "Wimbo huu niliufaham nikiwa darasa la tatu mwaka 2000, hadi leo na uzee wangu wote huu siwezi kuusahau. Enzi zile tuliimba kwa kujifurahisha tu ila sasa nimegundua una maana kubwa sana katika kizazi cha watu wanaofuga ujinga.
 
Mabata madogo dogo yanaogelea x2 katika shamba zuri la bustani
Yanapenda kutembea bila viatu x2 katika shamba zuri la bustani
Wanapenda lia lia kwa kwa kwa kwaaa x2 katika shamba zuri la bustani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…