Nyimbo ya Tabasam by mr blue ft steve na q chief

Nyimbo ya Tabasam by mr blue ft steve na q chief

wakuu natafuta nyimbo ya mr blue ile tabasam yenye version ya Q chief. Kila nnayoona kipande cha Q chief kimeondolewa. Mwenye nayo tafadhali. Mim kijana wa zamani nikumbukie enzi yetu
Ni kweli hicho kipande alichoimba Q Chief kwenye hiyo nyimbo, kimeondolewa

Sijui kwanini walifanya hivyo
 
wakuu natafuta nyimbo ya mr blue ile tabasam yenye version ya Q chief. Kila nnayoona kipande cha Q chief kimeondolewa. Mwenye nayo tafadhali. Mim kijana wa zamani nikumbukie enzi yetu
Hadi Mimi naitafuta hiyo version siipati ni sehem ndogo tu ila chila Kuna namna aliua mle.

ila story ya hiyo Ngoma ilipikwa kwa man water Original version kabisa ilikuwa ni ya Blue na q chilla

Kipindi icho Steve anaendaga kwa Man water katoa Ngoma kadhaa ambazo hata hazijapenya mjini

kwahyo kabla Ngoma haijawa released Man water akamcheki Steve RNB kuwa Kuna Ngoma ya Blue hapa ila Haina chorus njoo uingize

Kumbuka hapo Ngoma ilishaisha tangu mda na Steve akuambiwa kuwa hiyo Ngoma Kuna chorus ya mtu mbaya Q chila kuwa alishaifanya, yaani Man water hakumskilizisha kabisa (nafikiri angejua Steve kuwa Mzee Chila alipita sidhani kama Steve angepata nguvu ya kuua vile)

Bhasi bhana Steve alipoambiwa Ngoma ni ya Blue na yeye ni Underground mda huo, bhana bhana ikawa tatizo ilo njaa zote akamalizia hapo, alijua hili ndio tobo sasa.

Baada ya Steve kuingiza maunyama yake bhana wewe man water kamchek blue kumjulisha Ile version ya Steve duh blue alichanganyikiwa na kuipitisha Ile ya Steve

Unaambiwa Mzee Chila alimaimdi vibaya mbaya yaani ukisikiliza version ya Blue na Steve Bado Kuna vocal za mwisho ya chila ila aliambiwa aje shooting kichupa akasusa Mzee mzima.
 
Back
Top Bottom