Nyimbo za Tanzania zatumika kuhamasisha maandamano Kenya

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Hii ni katika maandamano yaliyopigwa marufuku na serikali ya Ruto leo.

Katikati ya Nyomi hilo Kibra Nairobi, ni Raila Amolo Odinga (Baba) akiwa kazini. Kwa hakika hakuna mwingine kama yeye:

Nyuma ya shughuli ni goma zito kutokea Tanzania, "hakuna kama yeye." Kweli kwenye miti hakuna wajenzi.

Anakamatwa vipi Odinga ndani ya nyomi hilo?

Mungu si Athumani matumizi ya nyimbo hizi hayawezi kuacha kuwa mashamba darasa. Siku moja yatasikika kutokea makwetu Nanjilinji Kilwa, huko.

Heko kwao watunzi wa wimbo huu kwani kwa hakika wamewakilisha.
 
Mambo gani?
Umeme kukatika hovyo, maji ya mgao, bidhaa muhimu kupanda bei, ufisadi, semina, hafla za pongezi na ziara zisizo na tija zinazokandamiza watanzania, ulambaji wa asali (kula kwa urefu wa kamba) tozo zinazoumiza watanzania, mikopo isiyo na ulazima n.k ni mambo mengi sana ya hovyo yanayozidi kukandamiza wananchi, hususan wa hali ya chini.
 
Tungekuwa na upinzani dhabiti sa hv tusingekuwa tunaibiwa twiga live live , tuna kundi la hovyo linalojiita upinzani huku likila sahani moja na matapeli na linazibia njia kwa upinzani dhabiti kuimerge
Wameporwa majimbo yote uliandamana? Hawapo bungeni wamebaki mafisadi watupu alafu unataka upinzani wafanye Nini sasa Cha ajabu kama nyie wenyewe hamkuona umuhimu wao kuwa bungeni?

Kama mmeridhika na majimbo na halmashauri zote kuwa chini ya CCM nendeni mkalalamike makao makuu ya CCM. Haiwezekani ujinga wa chama kingine lawama wapewe chama kingine.

Ni sawa na Mama Yako kakutelekeza alafu unaenda mlaumu baba wa Nyumba jirani kwanini hakumuoa mama Yako ndio maana unapitia shida? Does it make sense.
 
Umeme kukatika hovyo, maji ya mgao, bidhaa muhimu kupanda bei, ufisadi, semina, hafla za pongezi na ziara zisizo na tija zinazokandamiza watanzania, ulambaji wa asali (kula kwa urefu wa kamba) tozo zinazoumiza watanzania, mikopo isiyo na ulazima n.k ni mambo mengi sana ya hovyo yanayozidi kukandamiza wananchi, hususan wa hali ya chini.

Wanajifanyaga hamnazo ila ipo lugha wanayoielewa vyema zaidi:

Hii ni katika maandamano yaliyopigwa marufuku na serikali ya Ruto leo.

Katikati ya Nyomi hilo Kibra Nairobi, ni Raila Amolo Odinga (Baba) akiwa kazini. Kwa hakika hakuna mwingine kama yeye:

View attachment 2567989

Nyuma ya shughuli ni goma zito kutokea Tanzania, "hakuna kama yeye." Kweli kwenye miti hakuna wajenzi.

Anakamatwa vipi Odinga ndani ya nyomi hilo?

Mungu si Athumani matumizi ya nyimbo hizi hayawezi kuacha kuwa mashamba darasa. Siku moja yatasikika kutokea makwetu Nanjilinji Kilwa, huko.

Heko kwao watunzi wa wimbo huu kwani kwa hakika wamewakilisha.
Mungu awabaliki sana waandamanaji wapate haki yao.Hakika nawapenda na kuwakubali sana wakenya.Sisi tumekalia uchawa tu.
 
IMG_20230327_222800.jpg
 
Back
Top Bottom