NYIMBO ZINAZOISHI (LIVING SONGS) ZA PROFESSOR JAY.

RD07

Member
Joined
May 5, 2024
Posts
52
Reaction score
90
Habari wana JF;
Leo nikasema ngoja nisikilize kidogo nyimbo za zamani kuanzia 2010 kurudi nyuma, nikaingia mtandaoni kuzipakua hasa zile nilizokuwa nazipenda...
Sikuacha za Professor Jay, nikachukua kadhaa zikiwemo NDIO MZEE, KIKAO CHA DHARURA na NANG'ATUKA...
Asee jamaa yale aloyaimba mule ndio wanayotifanyia Wanasiasa wetu zama hizi. Yaan ule uongo aloimba mule kwenye "Ndio Mzee" hadi Kupewa kura na kuingia Madarakani na baada ya miaka 5 akarudi tena kwa Wananchi na kuwapooza kwa ahadi za kwamba "Kiufupi nimezongwa sana na haka kamuda, mkiniongeza tena muda nitatekeleza yote niliyosema"😄
Kuna Mwamba alocheza miguu yote mule wakuitwa MC BABU AYUBU (Huyu jamaa sijui kapotelea wapi) ambaye ndo aliingiza zile sauti za wananchi ikiwemo; "Naitwa Sajent General.... Nlikuwa nauliza zile Helkopter zetu vipi?" Akajibiwa (Nimepanga kuanzisha kwanza Chuo cha Marubani ili kuepusha ajali nyingi sn angani, baiskeli huwez kuendesha Helkopter utaendeshaje?) afande akakausha.
Mwananchi akauliza "Mheshimiwa mabomba ya maziwa nchi nzima" Mhe. Akamkatisha (Jamani hebu ulizeni maswali ya kiutu uzima, mabomba ya maziwa nchi nzima hilo swala haliwezekani, mlinielewa vibaya nasisitiza haliwezekani, yaan utadhani hakuwaahidi🤣).. Mwananchi mwingine akauliza "Mhe. Ulituahidi tutagawana vyakwako, kwenye kampeni zako ilikuwa n moja ya ahadi zako?", Mheshimiwa akacharuka (Kugawana vyakwangu??? Hiyo haiwezekani, Familia inantazama nina majukumu, imeandikwa kila mbuzi atakula kwa urefu wa kamba yake, halafu mbona kama mnaniuliza maswali mengi ya kunikomoa?,) yaan keshasahau kuwa aliahidi mwenyewe kuwa hali ikiwa ngumu atagawana vyakwake na wananchi. Mwisho anauliza kuna mwngne anaswali aulize?, Wananchi wanamtukana kimoyomoyo tuu, nae anawauliza naona maswali yameisha na hyo inaonyesha mpo tayar kunipa kura, Wananchi kwa hasira wanamjibu AAH WAPI!, Ila haohao wananchi wakitoka hapo wanasahau siku ya kura wanampa tena kura zao na anarudi madakani. Wale Wananchi ndio sisi Watanzania na tabia zetu zimeonyeshwa mule, kuwa huwa tunapewa ahadi ambazo kwa akili ya kawaida tunajua kabisa kuwa haziwez kutekelezwa na Mgombea ila sisi ndo wakwanza kumpigia makofi mgombea kumpongeza bila kufikiria.
Akishapewa kura anaondoka anasahau wananchi had muda wa uchaguzi ukikaribia ndo utawaona wanarudi tena kuwalaghai Wananchi, na wanapewa tena kura wanarudi madarakani. Hao ndo WATANZANIA.
Prof. Jay aliimba nyimbo zinazoishi,
Na mwisho kabisa akamaliza na NANG'ATUKA, akielezea kujutia nafsi yake kwa kutumia madaraka yake vibaya kuumiza Wananchi wake, akibainisha kuwa alidiriki kuwapa connection vimada wake kuwapa vyeo, akielezea mabaya yote aloyafanya bila kuwajali wananchi ambayo yalisababisha Wananchi wake kuishi maisha magumu.
Hii inaonyesha dhahiri kuwa alitaka kufikisha ujumbe kuwa Kiongozi akisimama vizuri kwaajili ya Wananchi anaweza kuwafanya Wananchi wake kuishi vizuri na kuondoa ugumu wa maisha ktk jamii na kupunguza umasikini, lakn pia akiwa mbinafsi na mpenda rushwa basi anaweza kuwafanya Wananchi wake kuishi maisha magumu na kuongeza umasikini.

Ni nyimbo gani nyingine zilizoimbwa kitambo ila ujumbe wake unaishi hadi sasa?, (Living songs). Zitaje kwenye Comments.
Ahsanteni.
 
Alafu kuna hizi sa sa hivi unaambiwa PAKIA MATE ITELEZE, mara Kampitisha kwa mpalange.
Zinakera sana kiukweli, imewafanya hata Wasanii wenye akili nao kuacha kuielimisha jamii kupitia nyimbo na mistari nao wamehamia kwenye mziki biashara inawabidi waimbe ujinga ilimradi hadhira icheze ajaze shows
 
Si
Nani azipitishe

Ziwafunue akili

Hapo tu wakati wa kampeni Zina zimwa kimafia

Fuatilia uone kama Oktober zitapigwa!!
jui kwanini yeye mwenyewe hazitumiagi ili kumdhoofisha mpinzani anayegombea nae?
 
Hata kala jeremiah Alikuwa anaimba nyimbo nzuri sana
 
Kuna Chemsha Bongo mpaka kesho naisikiliza, alikula sana bata mle!
Mpuuuzi hakuwaza fyucha
Habari wana JF;
Leo nikasema ngoja nisikilize kidogo nyimbo za zamani kuanzia 2010 kurudi nyuma, nikaingia mtandaoni kuzipakua hasa zile nilizokuwa nazipenda...
Sikuacha za Professor Jay, nikachukua kadhaa zikiwemo NDIO MZEE, KIKAO CHA DHARURA na NANG'ATUKA...
Asee jamaa yale aloyaimba mule ndio wanayotifanyia Wanasiasa wetu zama hizi. Yaan ule uongo aloimba mule kwenye "Ndio Mzee" hadi Kupewa kura na kuingia Madarakani na baada ya miaka 5 akarudi tena kwa Wananchi na kuwapooza kwa ahadi za kwamba "Kiufupi nimezongwa sana na haka kamuda, mkiniongeza tena muda nitatekeleza yote niliyosema"😄
Kuna Mwamba alocheza miguu yote mule wakuitwa MC BABU AYUBU (Huyu jamaa sijui kapotelea wapi) ambaye ndo aliingiza zile sauti za wananchi ikiwemo; "Naitwa Sajent General.... Nlikuwa nauliza zile Helkopter zetu vipi?" Akajibiwa (Nimepanga kuanzisha kwanza Chuo cha Marubani ili kuepusha ajali nyingi sn angani, baiskeli huwez kuendesha Helkopter utaendeshaje?) afande akakausha.
Mwananchi akauliza "Mheshimiwa mabomba ya maziwa nchi nzima" Mhe. Akamkatisha (Jamani hebu ulizeni maswali ya kiutu uzima, mabomba ya maziwa nchi nzima hilo swala haliwezekani, mlinielewa vibaya nasisitiza haliwezekani, yaan utadhani hakuwaahidi🤣).. Mwananchi mwingine akauliza "Mhe. Ulituahidi tutagawana vyakwako, kwenye kampeni zako ilikuwa n moja ya ahadi zako?", Mheshimiwa akacharuka (Kugawana vyakwangu??? Hiyo haiwezekani, Familia inantazama nina majukumu, imeandikwa kila mbuzi atakula kwa urefu wa kamba yake, halafu mbona kama mnaniuliza maswali mengi ya kunikomoa?,) yaan keshasahau kuwa aliahidi mwenyewe kuwa hali ikiwa ngumu atagawana vyakwake na wananchi. Mwisho anauliza kuna mwngne anaswali aulize?, Wananchi wanamtukana kimoyomoyo tuu, nae anawauliza naona maswali yameisha na hyo inaonyesha mpo tayar kunipa kura, Wananchi kwa hasira wanamjibu AAH WAPI!, Ila haohao wananchi wakitoka hapo wanasahau siku ya kura wanampa tena kura zao na anarudi madakani. Wale Wananchi ndio sisi Watanzania na tabia zetu zimeonyeshwa mule, kuwa huwa tunapewa ahadi ambazo kwa akili ya kawaida tunajua kabisa kuwa haziwez kutekelezwa na Mgombea ila sisi ndo wakwanza kumpigia makofi mgombea kumpongeza bila kufikiria.
Akishapewa kura anaondoka anasahau wananchi had muda wa uchaguzi ukikaribia ndo utawaona wanarudi tena kuwalaghai Wananchi, na wanapewa tena kura wanarudi madarakani. Hao ndo WATANZANIA.
Prof. Jay aliimba nyimbo zinazoishi,
Na mwisho kabisa akamaliza na NANG'ATUKA, akielezea kujutia nafsi yake kwa kutumia madaraka yake vibaya kuumiza Wananchi wake, akibainisha kuwa alidiriki kuwapa connection vimada wake kuwapa vyeo, akielezea mabaya yote aloyafanya bila kuwajali wananchi ambayo yalisababisha Wananchi wake kuishi maisha magumu.
Hii inaonyesha dhahiri kuwa alitaka kufikisha ujumbe kuwa Kiongozi akisimama vizuri kwaajili ya Wananchi anaweza kuwafanya Wananchi wake kuishi vizuri na kuondoa ugumu wa maisha ktk jamii na kupunguza umasikini, lakn pia akiwa mbinafsi na mpenda rushwa basi anaweza kuwafanya Wananchi wake kuishi maisha magumu na kuongeza umasikini.

Ni nyimbo gani nyingine zilizoimbwa kitambo ila ujumbe wake unaishi hadi sasa?, (Living songs). Zitaje kwenye Comments.
Ahsanteni.
Weka hapa hata tuwimbo tuwili tutatu
 
Back
Top Bottom