Nyoka aina ya Black Mamba mawindoni

Kuna sehemu kuna mto nilikuwa nataka nioge,nikaanza kupiga uluzi huku najiandaa kuvua nguo,ghafla naona mwamba anatokea kwenye kichaka kichwa kiko juu anakuja kwangu fasta,ilinibidi nikimbie kuokoa maisha yangu.Ambacho sikujua,ni ule mluzi ndio ulimuita au aliniona kuwa natishia tu usalama wake akaamua kunitokea...
 
Mluzi alitaka kujua sauti inatokea wapi mana unamkera yeye yuko kwenye starehe zake.
 
Eti yule mjinga wa South Afrika mwenye kupindi cha kukamata nyoka anawadanganya watu anamshika black mamba kwa mikono tu kule kwenye channel ya Nat Geo Wild
Sasa Huwa ni sinema ile mzee au ? Yale ma elimu tu mbona urambo kuna vichwa vinawakamata kwa ishu za kwenda kuwasukuma kwa wazee wa vilinge.
 
Moja ya nyoka hatari kabisa anaeitwa Black Mamba akiwa kwenye mawindo, wale wa Tabora wanamuelewa sana huyo mwamba kabisa.
View attachment 3221795
NYOKA mpuuzi sana huyo pumbavu zake.
Wachina kwa uchu wao utawakuta wanakimbiza nyoka huku wameshika chumvi, pilipili na kibiriti, lakini wakisikia Koboko hapo watahama kambi
 


Ningali mdogo hawa Koboko walikuwa wanatusumbua sana kijijini lakini tulikuwa tunawaua kwa mawe tu.

Brazili kuna nyoka hatari zaidi ya koboko ila wao wenyewe wanazungumza mpira na samba tu; hawana taimu na nyoka hao.
 
9- Koboko hutembea haraka sana akiwa juu ya ardhi. Anaweza kusafiri umbali mrefu kwa kasi ya maili hadi 12 kwa saa. Hivyo usijaribu kukimbia atakufukuza mpaka akugonge sehemu ya mwili wako.
MKuu nikila nduki na kukimbia kwa kukata makona makona atanifata kweli?
 
Morogoro wanaongoza kwa majoka
 
Hiyo namba 8 niliona nyegere anamkimbiza huyu mwamba fasta akamgeuza mshikaki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…