Nyoka aina ya Black Mamba mawindoni

Nyoka aina ya Black Mamba mawindoni

Hivi Badala ya kumpelekea jungu la uji kwanini asipuliziwe sumu kwa kutumia kipulizi chenye nguvu kinachoweza kurusha dawa umbali mrefu ( mt 20-30)?
Na pia nyoka wote akiwemo koboko hawana uwezo wa kuhimili dawa za kuulia wadudu, petroli, mafuta ya taa na hata maji yaliyo changanywa na chumvi.
Vyote hivyo vikigusa mwili wa nyoka anakimbia mbali.
Nijuavyo nyoka wote humuogopa binadamu ingawa mara chache koboko huleta vurugu karibu na makazi ya watu.
Na pia hutokea mara chache kama mnakutana kwa bahati mbaya mkashtukizana kila mtu akipita zake anakung'ata ili kujihami.

Lakini mara nyingi Koboko aliyetulia kwenye territory yake hana madhara mpaka umchokoze maana yeye anaanza kukuona kabla hujamuona.

Hata hivyo wafrika (hasa watanzania) tunampa sifa kemkem koboko ambazo nyingi kati ya hizo hana.
Koboko hana uwezo wa kunywa uji wa moto kama ilivyo kwa binadamu.

Yule jamaa wa South Africa "Snake city" akisikiliza simulizi za watanzania hataingia majumbani kuwadaka koboko na Cobra.
Jamaa anawakimbiza na kisha kuwadaka kama mijusi.
Labda Tabora kuna aina tofauti ya koboko.
Nakuhakikishia atachemka hawa nyoka wengi wanoongelewa wa hapa Tanzania ni nyoka wa kishirikina we uliona wapi nyoka anaingia kwenye uji na kutoka mzima na kuanza kumfukuza mtu..
Mi niliona hiyo habari kabisa na yule mganga yupo hospitali.
 
Back
Top Bottom