Nyoka havui gamba, Kobe havui ngozi!

Nyoka havui gamba, Kobe havui ngozi!

Ibrah

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2007
Posts
2,730
Reaction score
530
NYOKA
Nyoka hana gamba, ana ngozi,
Nyoka hujivua ngozi,
awe mpya, fisadi na mgomvi
Nyoka kujivua ngozi, hakuondoi hatari

Nyoka hana gamba, ana ngozi
siku akivua ngozi, sirini yuko gizani
sumuye huimarisha,
matendo mabaya kufanya
Nyoka kujivua ngozi, hakuondoi hatari

Nyoka hana gamba, ana ngozi
shimoni hujiegama, hatoki hata kwa konzi
ngozi ikishamtoka, zaidi huwa hatari
masihara hatataka, mkali kuliko awali
huwa fisadi, mfisidi na mkaidi
Nyoka kujivua ngozi, hakuondoi hatari

Nyoka hana gamba, ana ngozi
kujivua ngozi kazeeka, hana mapozi
ataka kuwa kijana asiyesogeleka
nje akitokea, hafai kusogelewa
Nyoka kujivua ngozi, hakuondoi hatari

KOBE
Kobe hana ngozi, ana gamba
uhai ameutosa, siku akivua gamba
uzima ameshaukosa, mwisho wake umefika
Kobe akivua gamba, uhai umeshamtoka

Kobe hana ngozi, ana gamba
Kobe akuvua gamba, umauti umemfika
ingawa mwendo mfupi, safariye hataifika
Kobe hana ngozi, ana gamba

Kobe akivua gamba, kila kitu hadharani
mauti yatamfika, siri zake zi-nuruni
jeuri itamtoka, atawekwa hukumuni
siku akivua gamba, hakika yu mashakani

Kobe hana ngozi, ana gamba
gamba kwake desturi, asiyotaka iacha
itakuwa kubwa huzuni , siku gamba akiacha
atajikuta hukumuni, desituri akiiacha
 
Back
Top Bottom