NADHARIA Nyoka mwenye muonekano kama wa jogoo ni wa kweli?

NADHARIA Nyoka mwenye muonekano kama wa jogoo ni wa kweli?

Taarifa hii ni nadharia tu, tumeitolea ufafanuzi kwa kadiri ilivyowezekana
Source #1
View Source #1
Imekaaje hii wakuu?
1787469117416.png
 
Tunachokijua
Kupita mitandao ya kijamii ikiwemo facebook kumekuwepo na pcha inayosambaa ikimuonesha nyoka mwenye muonekano wa jogoo kichwani na kuibua maswali mengi kwa wafuatiliaji juu ya uhalisia wa picha hiyo. Tazama hapa, na hapa.

Kupitia baadhi ya comments za wasmaji, baadhi wameeleza kuwa ni kweli aina hiyo ya nyoka ipo ambapo pamoja na hilo, nyoka hao wanatajwa kuwa hatari sana huku wakiwa wanatoa mlio kama wa Jogoo anayewika na kwa wa kike basi hutoa mlio kama tetea.

JamiiCheck imefuatilia picha pamoja na madai hayo na kubaini kuwa hayana ukweli wala uthibitisho wa kisayansi.

Kumekuwepo na simulizi zinazoelezea uwepo wa nyoka wa aina hiyo haswa maeneo ya Tanzania, Zambia, Malawi, Afrika Kusini, Msumbiji na Afrika ya Kati. Nyoka huyo anatajwa kuwa na urefu wa hadi futi 20.

Nyoka huyo alipewa jina la ‘Crowing Crested Cobra’ , simulizi zikiendelea kumtaja kuwa amekuwa na asili ya kushambulia viumbe vingine hususan binadamu kwa kumgonga kichwani kama walipenda kukaa juu ya miti.
1787469428625-png.3655479

Picha Darren Naish​

Uhalisia ni kuwa tafiti zilibaini kuwa hakujawahi kuwepo nyoka mwenye sifa hizo katika ulimwengu na badala yake huenda kutokana na uelewa mdogo ama kuchanganya nyoka pamoja na sauti za ndege wengine waliokuwa wakiwasikia.

Hivyo nyoka huyo aliyepewa majina ya asili kutokana na jamii husika kama vile jina Bubu, Inkhomi, Hongo, Songo na Mbobo anasalia kuwa nadharia tu na simulizi za kale. Kwani sambamba na hayo ikumbukwe kuwa Nyoka hana mfumo wa sauti unaomuwezesha kuwika kama jogoo.
Hii ni kama ilivyovuma kulikuwepo na binadamu aitwae unju bin unuki 😂
 
Back
Top Bottom