NYOKA ,ALAMA YA UKOMBOZI (UUNGU) au USHETANI
SEHEMU YA II
Na Da Vinci XV
NYOKA KATIKA MAANDIKO MATAKATIFU
Kama nlivyopata kuelezea huko juu Mungu alimtumia nyoka katika kazi zake tofauti tofauti, ambazo ziliwakilishwa na nyoka
Maandiko ya Mwanzo kabisa ambayo yanamtaja nyoka ni katika kitabu cha (Mwanzo 3:1)
Hapo Bwana anajaribu kumuelezea Nyoka alivyo mwerevu na alivyofanikiwa kumrubuni Hawa na Mumewe kuvunja amri ya bwana Muumba wao.
Usisahau bwana anamzungumzia nyoka kiumbe mwerevu kupita kiumbe yoyote pale bustanini.
Sehemu ya pili ndio inaonyesha nyoka kama tulivyopata kuijadili huko juu Muungu anatumia nyoka kudhuru lakini vilevile Alama ya nyoka kama Tiba Tazama ( Hesabu 21: 4-9)
4 -
Wakasafiri kutoka mlima wa Hori kwa njia ya Bahari ya Shamu; ili kuizunguka nchi ya Edomu, watu wakafa moyo kwa sababu ya ile njia.
5 -
Watu wakamnung'unikia Mungu, na Musa, Mbona mmetupandisha huku kutoka nchi ya Misri, ili tufe jangwani? Maana hapana chakula, wala hapana maji, na roho zetu zinakinai chakula hiki dhaifu.
6 -
Bwana akatuma nyoka za moto kati ya watu, wakawauma, watu wengi wakafa.
7 -
Watu wakamwendea Musa, wakasema, Tumefanya dhambi kwa sababu tumemnung'unikia Mungu, na wewe; utuombee kwa Bwana, atuondolee nyoka hawa. Basi Musa akawaombea watu.
8 -
Bwana akamwambia Musa, Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi.
9 -
Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi.
Naam, habari ya waisraeli na Musa nadhani wengi wetu tunaijua jinsi walivyokuwa wabishi juu ya Musa walishushiwa Chakula kutoka mbinguni na bado wakakikataa kifupi walikuwa na kashikashi kubwa sana na Musa na mungu wake vitimbi vya hali ya juu,
Andiko hilo linabainisha nyoka katika pande mbili kama Uponyaji na pande nyingine ni mwenye Kuleta madhara, Mungu aliwatumia waisraeli nyoka baada ya kumnenea vibaya Mungu na Musa ambae amewaokoa katika ardhi ya Utumwa na Kuwapeleka nchi ya Ahadi nyoka hao waliwauma na kusababisha vifo kwao lakini Baada ya Kugutuka Mungu akamwagizia dawa ya Nyoka hao ambayo ni sanamu ya Shaba ya Nyoka ambayo yoyote aitazamae ilimwokoa kutokana na Kifo. Hivyo hapa nyoka alitambulika kama Uponyaji.
Wakala wa madhara na Uponyaji ni nyoka, kifo na Uzima ni Nyoka. Lakini vyote hivi vilifanywa na Bwana Mungu Baba.
Naam
Sehemu ya Pili ni Musa alipoamriwa na mungu wake kwenda kwa Farao, kumpa elimu juu ya M/Mungu ili kuomukoa na kuwaokoa watu kutoka katika Upotofu , na ili somo liende sawasawa Mwenyezimungu alijaalia kwa Musa miujiza ambayo kwayo Huenda firauni angepata kutambua haki, Musa alitumia nyoka kama alama na Muujiza mbele ya Firauni na Wakati huo huo wachawi wa Firauni walitumia nyoka pia. Habari hii inapatikana katika biblia na Qur'an kwa Ujumla wake.
QUR'AN 20:17-
17 -
Na nini hicho kilichomo mkononi mwako wa kulia, ewe Musa?
18 -
Akasema (Musa) : Hii ni fimbo yangu; naiegemea na ninawaangushia majani kondoo na mbuzi wangu. Tena inanifaa kwa matumizi mengine.
19 -
Akasema: Itupe, ewe Musa!
20 -
(Musa) Akaitupa. Mara ikawa nyoka anaye kwenda mbio.
Hayo ni mazungumzo kati ya Nabii Musa na Mola Wake alipopewa dhima ya kwenda kumkabili Farao na Upotofu wake na habari ya Musa kwenye Qur'an ilianzia hapo badala ya M/mungu kumpa muujiza huu ambao kilichofwata Hadithi yake tunaijua Wachawi wa Firauni/farao walitupa nyoka zao kushindana na Musa ambaye nae kwa uwezo wa M/Mungu aliwavaa wote na kuwameza nyoka wote wa wachawi , kilichofuata hapo kwa Wachawi ni kufuata Mungu wa Musa na kumuamini Musa ukitaka kupata kisa hiki Endelea katika Aya za Mbele za Sura hii ya 20 ndani ya Qur'an tukufu (Surat Taha)
Na kwenye Biblia habari hii inapatikana katika Kitabu cha (KUTOKA 7:9-) kinaelezea vyema jinsi fimbo(Nyoka) ya Musa na Haruni ilivyomeza Nyoka wote wa wachawi wa Farao rejelea andiko hilo.
Hapo nyoka ametumika kama Uchawi (Wachawi wa Farao) na Pia ametumika katika Ukombozi(Nyoka wa Musa),mapambano mawili haya kati ya Upande Mungu na Upande wa Shetani na wote wakiwakilishwa na Nyoka.
Ukiachana nyoka kuonekana kama mkombozi lakini upande wa pili ndani vitabu hivi vitatifu vinamtaja nyoka kama Shetani na Ibilisi na Upotofu , Sehemu ya kwanza kabisa ni pale ambapo nyoka alifanikiwa kumrubuni Mama yetu Hawa na Kumhadaa akafanikiwa kuvunja alichoamriwa na Mungu wake. (MWANZO 3:4)
Lakini pia Yohanna mtoto wa Zebedayo yule mwanafunzi wa Bwana Yesu, aliyetekwa na kupewa mateso katika kisiwa cha Patmo ili kumshurutisha aache kutangaza neno la M/mungu basi M/Mungu akamshushia ufunuo kumfunulia siri nyingi za dunia zijazo na zilizopita na zilizokuwepo wakati huo ili kumfariji Mwanafunzi huyu wa Bwana Yesu baada ya Kufikia hatua ya kukata tamaa juu ya mateso kutoka kwa Watesi wake.
Ufunuo wa Yohanna (12:9) inamtaja Nyoka kama Ibilisi /Shetani
(Ufunuo wa Yohana ) 12 : 9 -
Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.
Ukirudi juu kidogo hadi mstari wa Tisa unajaribu kumuelezea Nyoka huyu Ibilisi anapojaribu , kupambana na Jeshi la M/Mungu na mwisho kutupwa na jeshi lake lote kushindwa.
Ili kujaribu kuhalalisha utambulisho wake wa uwongo kama mungu. Hii ndiyo sababu Shetani alichagua kutumia ishara ya nyoka kama njia bora zaidi ya kumdanganya Hawa na vilevile uzao wake kuanzia wakati huo na kuendelea.
Maandiko yanatusaidia kuona kwamba Shetani anaiga na kupotosha kila ukweli wa kimungu, kila dhana ya kimungu, kanuni, au utendaji, kila ishara nzuri na chanya, picha, ishara, na alama ili kudanganya na kuendesha roho za watu.
Na ndio sababu hii hata miungu , ya Watu wa kale na jamii za zamani zilitumia Ishara ya Nyoka kama njia ya kuyafikia mafanikio ya kiuungu na kama ujuavyo Mfumo na mwenendo wa miungu wengi ni mwenendo wa Shetani.
Kwa maana Nyoka mwanzo ilisimama kama Alama ya Kiungu na Uponyaji kutoka Mungu.
DaVinci XV