Habari ndugu wananchi,
Kuna uzushi uliozoeleka hapa Tanzania kuwa "kinachosababisa NYOKA wa kijani kuanguka chini kutoka juu ya mti ambao chini yake Kuna watu wanapiga stori NI umbea, kwamba alikuwa akisikiliza stori zao kwa muda mrefu kwa kujificha hivyo zimemnogea na ameshindwa kuendelea kujificha, "
Jamiichek fanyeni kitu hapa, hi ni kweli au uzushi?
Kuna uzushi uliozoeleka hapa Tanzania kuwa "kinachosababisa NYOKA wa kijani kuanguka chini kutoka juu ya mti ambao chini yake Kuna watu wanapiga stori NI umbea, kwamba alikuwa akisikiliza stori zao kwa muda mrefu kwa kujificha hivyo zimemnogea na ameshindwa kuendelea kujificha, "
Jamiichek fanyeni kitu hapa, hi ni kweli au uzushi?
- Tunachokijua
- Nyoka yupo kundi la reptilia wasio na miguu. Kuna takriban spishi 3,000 duniani. Nyoka wana damu baridi na ngozi ya magamba. Wote ni wala nyama na spishi mbalimbali hutumia sumu kwa kuwinda lakini nyoka walio wengi hawana sumu wanashika windo kwa miili yao au kwa mdomo tu. Kuna nyoka wadogo wenye sentimita kumi tu wakiwa wazima na nyoka wakubwa hadi urefu wa mita 7.6.
Nyoka wa kijani ni mwembamba Kwa ukubwa, huainishwa kama nyoka "mdogo wa wastani", anayefikia 36-51 cm (14-20 inch) kwa jumla ya urefu (pamoja na mkia) akiwa mkubwa. Nyoka mrefu zaidi laini wa kijani alipimwa kuwa na urefu wa sm 66 (inchi 26). Mkia huo hufanya takriban 1/4 hadi 1/2 ya urefu wa jumla wa nyoka; wanaume wana mikia mirefu kuliko wanawake.
Kuna aina nyingine ya nyoka wa kijani ambao ni kijani kibichi kwenye mgongo wake, na tumbo la manjano au nyeupe, na wana magamba laini ya mgongo, tofauti na wale nyoka wa kijani kibichi, ambao wamejikunja. Mizani yake laini ya uti wa mgongo imepangwa katika safu 15 katikati.
Je, ni kweli nyoka wa kijani ni wambea na hupenda kusikiliza maongezi ya watu?
Kwenye chapisho la BBC Swahili lilieleza kuhusu nyoka kutokua na masikio, Limesema, Kuna kauli kwamba mtu anayeweza kusikia sauti ndogo za chini inasemekana ana masikio kama ya nyoka. Hata hivyo, Hii haina maana kwamba nyoka wana masikio. Kwa kweli, nyoka hawana masikio yanayoonekana kwa nje. kwa kuwa hawana masikio kama ya wanadamu, hawawezi kusikia sauti moja kwa moja.
Nyoka hawana sikio la nje, lakini wana sehemu zote za sikio la ndani kama tulizonazo. Mishipa yao—inayoitwa “columella”—ni tofauti kidogo na yetu kwa kuwa inaunganishwa na mfupa wa taya, na kuwawezesha kuhisi mitetemo. Hata hivyo, wanaweza kusikia tu sehemu ya sauti tunazosikia. Nyoka wanaweza kutambua mitetemo kati ya Hertz 50 na 1,000, ilhali wanadamu wanaweza kusikia kati ya Hertz 20 na 20,000.
Katika kutafuta ukweli zaidi JamiiCheck Ilizungumza na Tito Lanoy Mkufunzi Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori - Mweka, ambaye amesema;
"Kuna aina nyingi sana za nyoka wa kijani hapa Tanzania. Miongoni mwao aina mbili wana sumu kali. Nyoka wa kijani wanaoongelewa sana na watu ni wale wanaokaa kwenye maua na fensi za michongoma. Ukubwa wao ni chini ya mita moja".
Kuhusu nyoka kusikiliza Umbeya, Tito Lanoy anakanusha hoja hiyo kwa kusema kuwa :-
Kuhusu nyoka kupenda kusikiliza umbea siyo kweli sababu moja kubwa ni kuwa nyoka hana masikio hivyo basi hawezi kusikia sauti. Nyoka husikia kwa mwili wake kudaka mitetemo ardhini na huelewa kwa kutumia harufu, ndio maana wakati wote nyoka hutoa ulimi nje kukusanya harufu na hutafsiriwa na organ zijulikanazo kama Jacobson.
Macho ya nyoka yana uono hafifu hivyo basi wakati mwingi anategemea mitetemo na harufu.Kwasababu ya hawa nyoka kukaa karibu na binadamu hujikuta wamezoea yale mazingira na kukaribiana na binadamu bila hofu.Ndio maana wanajikuta matatani wanapoonekana na binadamu"
Kutokana na nyoka kukosa masikio ya nje yanayoweza kusikia kama tulivyo binadamu, JamiiCheck imejiridhisha kuwa nyoka wa kijani hawana tabia ya kusikiliza maongezi ya watu bali huwa wanakuwa na maisha yao ya kawaida wakiwa juu ya miti kutokana na kuishi mazingira ya karibu na binadamu, hivyo hoja ya kusikiliza umbeya ni uzushi.