PreGE2025 Nyongo atangaza kuwania tena ubunge, awataka wagombea wenzake wajipange

PreGE2025 Nyongo atangaza kuwania tena ubunge, awataka wagombea wenzake wajipange

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mwanantogakulya

Senior Member
Joined
Mar 18, 2025
Posts
157
Reaction score
155
Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Stanslaus Nyongo, ametangaza rasmi nia ya kuwania tena ubunge wa jimbo hilo kwa kipindi cha tatu mfululizo katika uchaguzi mkuu ujao.

Nyongo amesema amefikia uamuzi huo baada ya kutathmini maendeleo yaliyopatikana chini ya uongozi wake tangu alipochaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2015.

“Wananchi wa Maswa Mashariki wameshuhudia maboresho ya huduma za afya, elimu, miundombinu ya barabara na maji. Haya si maneno, ni ukweli unaoonekana kwa macho,” alisema Nyongo huku akishangiliwa na wananchi waliohudhuria mkutano huo.

Nyongo alitaja baadhi ya miradi mikubwa iliyotekelezwa kuwa ni ujenzi wa zahanati na vituo vya afya katika vijiji vilivyokuwa havina huduma hizo, upanuzi wa shule za sekondari, pamoja na ujenzi wa barabara za vijijini kwa kiwango cha changarawe na kiwango cha lami mjini Maswa.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Aidha, alitumia fursa hiyo kuwaonya wanaowania kiti hicho katika uchaguzi ujao, akisema:
“Wajipange vizuri. Kuongoza jimbo hili si kazi ya lelemama. Watu wanahitaji maendeleo, na si majungu na si kila mtu anaweza kuyaleta. Sina shaka kuwa wananchi wataendelea kuniamini kutokana na kazi niliyofanya.”amesema

Katika siku za karibuni, kumekuwa na taarifa za baadhi ya wanachama wa chama tawala kuonyesha nia ya kutaka kuwania nafasi ya ubunge katika jimbo hilo, hali inayotarajiwa kuongeza ushindani katika uchaguzi ujao.

20250511_172009.jpg
 
Back
Top Bottom