SI KWELI Nyongo ya mamba ni sumu inayoweza kuua

SI KWELI Nyongo ya mamba ni sumu inayoweza kuua

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Naomba kuuliza wataalamu wa jamii check. Maisha yangu yote naamini kuwa nyongo ya mamba ni sumu, lakini kuna bosi wangu mmoja tumebishana vikali akidai kuwa si sumu bali ni nyongo tu kama ya binadamu. Ukweli ni upi?
crocodile.jpg
 
Tunachokijua
Kwa miaka kadhaa nyongo ya mamba imekuwa ikitajwa kuwa chanzo cha vifo vya watu, ambapo watu wengi wakiamini kuwa nyongo ya mamba ni sumukwa binadamu.

Januari 2015 nchini Msumbiji, watu 25 walitangazwa kufariki ambapo redio zilitangaza vifo hivyo kusababisha na nyongo ya mamba.

Hata hivyo, JamiiForums baada ya kupitia maandiko kadhaa ya wataalamu akiwemo Profesa Norman Nyazema ambaye ni mbobezi wa fani ya famasia, amekanusha imani maarufu hii baada ya kufanya utafiti wa kina wa jambo hilo.

Prof Nyazema, ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Limpopo nchini Afrika Kusini, amethibitisha kuwa nyongo ya mamba haina sumu kabisa, hata hivyo huwa inakausha na kuuzwa China kama dawa ya kuongeza hamu ya kushiriki tendo la ndoa

“Nyota ya mamba haina sumu hata kidogo. Kwa kweli, inakaushwa kwenye shamba la mamba huko Kariba na kusagwa kabla ya kuuzwa Uchina ambako inatumika kama dawa ya kuongeza hamu ya kushiriki tendo la ndoa,” Nyazema alisema.

Alisema alikuwa amefanya uchunguzi ambapo alitaka kugundua dalili zinazowakabili wale "waliotiwa sumu" na nyongo na ikiwa kunaweza kuwa na dawa ya sumu hiyo, alipogundua kuwa nyongo hiyo haina madhara.

Katika wasilisho la utafiti wake alisema iko miti ambayo ina sumu kali na hutumiwa na waganga wa kienyeji katika kuua watu katika matukio ya kunywa pombe kwa Pamoja ambayo ndio matukio yanayoripotiwa mara kwa mara.

Hata watu waliokufa nchini Msumbiji baada ya kunywa pombe yenye sumu, pombe waliyotumia ilithibitisha kuwa sumu iliyokuwa kwenye pombe ile haikuwa nyongo ya mamba.
Hebu tuongelee enzi za KMCL, na yule mzungu anaiitwa bongoman
Na ile timu ya mpira ilikuwa inatunzwa vizuri
Usinikumbushe Skanska na zile Scania zao, zinapigwa kidebe huku zinatembea
Nilipita hapo Tanzoro Drilling kama unaikumbuka
Zote nazikumbuka. Kwenye kibasi Kakola..!!
 
mamba hata hapa tanzania analiwa.nenda mbinga/nyasa huko, na maeneo mengine yenye mamba. ziwa tanganyika etc. mamba akifa tu cha kwanza huwa ni kuondoa nyongo na kuizika. nyama inaliwa. ulaya inaliwa kama kawaida. uchina ni chakula kizuri tu.
 
Swali ni hili; kama nyongo yake ni sumu na imo tumboni mwake ikitumika kusaga mafuta kwanini isingeanza kumuua yeye mwenyewe??--- kazi ya nyongo kwa wanyama wote ni kazi moja tu ya kusaga mafuta yanayoingia tumboni kana chakula hivyo kama nyongo ya mamba ingekuwa ni sumu basi hata Nyongo za Binadamu, Ng'ombe, kuku, Mbuzi nk nazo pia zingekuwa ni Sumu.
Kitu kinachoua kiumbe kimoja si lazima kiue kiumbe kingine, kama ambavyo binadamu hawezi kula vitu anavyokula mamba, basi vivyo hivyo nyongo ya mamba haiwezi kuwa sawa na ya binadamu
 
Kitu kinachoua kiumbe kimoja si lazima kiue kiumbe kingine, kama ambavyo binadamu hawezi kula vitu anavyokula mamba, basi vivyo hivyo nyongo ya mamba haiwezi kuwa sawa na ya binadamu

Kazi ya nyongo in genearal kwa viumbe wote wenye nyongo ni ipi??, Tuanze na swali hilo.
 
Huyo aliyesema ni uzushi,sidhani kama alielewa swali,aisee mbaya zaidi akasema inakaushwa na kuuzwa kama dawa ya nguvu za kiume, aisee,alikua na ajenda ya kutuua nini?
Hadi kesho,mamba akiuawa,nyongo yake huwa chini ya uangalizi ili isije ikachukuliwa na wakora,wakaitumia kuua binadamu wenzao.
 
Mamba analiwa,ila nyongo yake huondolewa na kufukiwa au kutupwa kwenye kina kirefu cha maji,tena kukiwa na usimamizi mkubwa.Huyo mhadhiri sijui kafanyia tafiti kwa mamba wa wapi?
Aje Nyasa au ziwa Rukwa afanye upya utafiti.
mamba hata hapa tanzania analiwa.nenda mbinga/nyasa huko, na maeneo mengine yenye mamba. ziwa tanganyika etc. mamba akifa tu cha kwanza huwa ni kuondoa nyongo na kuizika. nyama inaliwa. ulaya inaliwa kama kawaida. uchina ni chakula kizuri tu.
 
Nami nimesikia Sana Simulizi kuhusu Nyongo ya Mamba, wanasema ukiweka kwenye Maji ni ColourLess(Haitoi Rangi) na wameenda mbali zaidi kwamba vilevile ni TasteLess(Haina Ladha). Wabobezi njooni huku Mtiririke kutujuza kuhusu Nadhalia hizi za NYONGO ya MAMBA!!
Nyongo sio nyama
 
Swali ni hili; kama nyongo yake ni sumu na imo tumboni mwake ikitumika kusaga mafuta kwanini isingeanza kumuua yeye mwenyewe??--- kazi ya nyongo kwa wanyama wote ni kazi moja tu ya kusaga mafuta yanayoingia tumboni kana chakula hivyo kama nyongo ya mamba ingekuwa ni sumu basi hata Nyongo za Binadamu, Ng'ombe, kuku, Mbuzi nk nazo pia zingekuwa ni Sumu.
Sumu ikiwekwa sehemu yake haiuwi..!! Unadhani kwanini sumu ya nyoka haimuuwi yeye mwenyewe? Wewe mwenyewe hapo ulipo kinyesi chako kikitoka tumboni na kuingia kwenye moyo unaweza sepa fasta
 
Nyongo hua kali sana mbona mtu ale nyongo.Kwa wanyama wote kuku ,mbuzi ,ngombe hatukuli nyongo tunatupa
 
Naomba kuuliza wataalamu wa jamii check. Maisha yangu yote naamini kuwa nyongo ya mamba ni sumu, lakini kuna bosi wangu mmoja tumebishana vikali akidai kuwa si sumu bali ni nyongo tu kama ya binadamu. Ukweli ni upi?
crocodile.jpg
MImi supu bila ya kuchanganyia nyongo ya mamba huwa haipandi
 
Sumu ikiwekwa sehemu yake haiuwi..!! Unadhani kwanini sumu ya nyoka haimuuwi yeye mwenyewe? Wewe mwenyewe hapo ulipo kinyesi chako kikitoka tumboni na kuingia kwenye moyo unaweza sepa fasta

Wala huelewi somo, Sumu ya nyoka ipo kwa ajili ya kutafutia mawindo isitoshe pia ni kwa ajili ya kujilinda na adui zake, mawindo na adui zake vyote vipo nje ya mwili wake na hiyo sumu huhifadhiwa katika venom gland , kinyesi chenyewe huwa ni makapi baada ya chakula kufyonzwa viini vinavyotakiwa na mwili (assimilated) kiasi kwamba kinyesi kinageuka kuwa ni kitu kisichofaa tena kikirudishwa tena tumboni hii mfano wake ni sawa na Petrol na moshi katika gari, petroli ikishaunguzwa ndani ya injini na ikageuka kuwa moshi basi huo moshi hauwezi kutumika tena kama petrol mfano huu ni sawa na chakula na kinyesi kwa wanyama.

Tuje kwenye nyongo, Nyongo ipo kwa viumbe vyote hai vinavyokula mafuta na vyakula vyenye mafuta, nyongo zote zina sifa na tabia moja ya kikemikali, sifa ni; 1--Uchungu, 2--kimiminika, tabia ni 1--kusaga mafuta, 2-- Kuchanganyika na mafuta iliyoyasaga na kuwa kitu kingine..

Swali la kujiuliza ni; Mafuta yakisha sagwa na nyongo kinafuata kitu gani??--- kinachofuata ni huo mmeng'enyo (kitu kilichopatikana baada ya nyingo kufanya mmeng'enyo) kufyonzwa kama nutrient na kuingizwa kwenye damu ya mnyama, kumbuka hiyo hali ipo kwa viumbe vyote vyenye nyongo, sasa inakuaje nyongo ya mnyama fulani inakuwa ni sumu lakini nyongo hiyo hiyo kwa mnyama mwingine sio sumu wakati nyongo zote zinafanana na zinafanya kazi moja?!.

Hakuna utafiti wa kisayansi uliowahi kufanywa na kuandikwa kwamba nyongo ya mamba wa aina yoyote ni sumu, kumbuka duniani kote kuna aina mbalimbali za mamba na wala huwezi kusikia ikisemwa kwamba nyongo ya mamba ni sumu isipokuwa huku kwetu Africa ya mashariki na sehemu yake ya kusini ndio utasikia huo uvumi.
 
Naomba kuuliza wataalamu wa jamii check. Maisha yangu yote naamini kuwa nyongo ya mamba ni sumu, lakini kuna bosi wangu mmoja tumebishana vikali akidai kuwa si sumu bali ni nyongo tu kama ya binadamu. Ukweli ni upi?
crocodile.jpg
Kumbe nyongo ya mamba ni dawa ila zamani nakua nilisikia ni sumu.
 
Back
Top Bottom