Nyota 5 'wa Kimataifa' wa Simba SC kulitetemesha bara La Afrika.

Nyota 5 'wa Kimataifa' wa Simba SC kulitetemesha bara La Afrika.

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Kipindi ile breki ya kupisha mechi za kimataifa ikiianza leo, wachezaji watano wa kimataifa toka Simba SC wanatarajia kulitetemesha Bara la Africa, pale watakapokua katika viwanja mbali mbali kuyatumikia mataifa yao.

Jina la mchezaji, Timu yake, Mda wa mechi ni kama ifuatavyo;
1. Yule kiungo anayetumia akili na ufundi mwingi uwanjani, uwezo mkubwa wa kupiga chenga, miguu miepesi, maono na pasi zenye macho, Clatous Chama, ataliwakilisha taifa lake la Zambia.

Tarehe: 10/10/2018
Mechi: Zambia 2-1 Guinea-Bissau (FT)


Tarehe: 14/10/2018
Mechi: Guinea-Bissau 2-1 Zambia (FT)


2. Yule kiungo mshambuliaji ambaye mechi ya mwisho akiitumikia klabu yake, alicheza dk 13 tu huku akipiga mipasi 27 ambapo hakuna hata 1 iliyopotea Haruna Niyonzima pamoja na mshambuliaji bora kabisa kwa sasa katika ukanda wa EAC Meddie Kagere watashuka dimbani kulitumikia taifa lao la Rwanda.

Tarehe: 12/10/2018
Mechi: Guinea 2-0 Rwanda (FT)


Tarehe: 16/10/2018
Mechi: Rwanda 1-1 Guinea (FT)


3. Yule 'CR7 wa Uganda' Okwi ambae katika mechi iliyopita ya TPL dhidi ya African Lyon aling'ara vilivyo pamoja na yule beki kisiki 'Kiboko ya Samata' Juuko Murshid wataliwakilisha taifa lao la Uganda.

Tarehe: 13/10/2018
Mechi: Uganda 3-0 Lesotho (FT)


Tarehe: 16/10/2018
Mechi: Lesotho 0-2 Uganda (FT)
 
Safi sana, nawatakia heri wasiumie warudi salama kuja kuitumikia Simba
 
Wanaenda kusugua benchi. Vipì safar hii utaishangiļa Cape Verde
Mkuu hao wote niliotaja makocha wao wanapoanza kuandika vikosi vyao huanza nao.. Kuthibitisha hili tunaanza na Chama saa 18:30 leo.
Kwangu mimi.. Simba SC kwanza mengine badae. As long as kuna Tz 1 Manula, 'Mwalimu wa Feisal' Mkude, Kapombe na Bocco tutakua pamoja.
 
Mkuu hao wote niliotaja makocha wao wanapoanza kuandika vikosi vyao huanza nao.. Kuthibitisha hili tunaanza na Chama saa 18:30 leo.
Kwangu mimi.. Simba SC kwanza mengine badae. As long as kuna Tz 1 Manula, 'Mwalimu wa Feisal' Mkude, Kapombe na Bocco tutakua pamoja.
Mkuu nasikia mkude kabaki et nimajeruhi maana nimesoma kwa sale jembe
 
Mechi Ndo inaanza hapa National Heroes Stadium.. Ni Zambia vs Guinea-Bissau

Kikosi Cha Kwanza Cha Zambia.
1. Kennedy Mweene
2. Solomon Sakala
3. Stoppilla Sunzu
4. Kabaso Chongo
5. Lawrence Chungu
6. Nathan Sinkala
7. Enock Mwepu
8. Clatous Chota Chama
9. ubambo Musonda
10. Augustine Mulenga
11. Justin Shonga
Sub:
1. Toaster Nsabata
2. Gideon Sichone
3. Isaac Shamujompa
4. Salulani Phiri
5. Rainford Kalaba
6. Patson Daka
7. Fashion Sakala
8. Bruce Musakanya
9. Lazarous Kambole

Kikosi Cha Kwanza Cha Guinea-Bissau
1. Jonas Asvedo Memdes
2. Eliseu Soares
3. Edigerson Gomes
4. Juary Marinho Soares
5. Bocak Balde
6. Manconi Soriano Mane
7. Jose Luiz Lopes
8. Francesco Santos
9. Tony Silva
10. Carlos Apna Eubalo
11. Frederic Mendy

Cc Prince Kunta
 
Dk 11: Zambia 0-0 Guinea-Bissau

Ila anachokifanya Chama si salama kwa afya ya wapinzani wake.
 
Dk 32: Zambia 1-0 Guinea-Bissau

Zambia wanaendelea kulisakama lango la Guinea kama Nyuki
 
Back
Top Bottom