KENGE 01
JF-Expert Member
- Mar 12, 2021
- 1,705
- 4,217
Na kenge,
Baada ya Cristiano Ronaldo kutua ligi ya waarabu saudi Arabia,Mastaa wengi wa ulaya wameonesha kuvutiwa na ligi hiyo kutokana na ushindani na pesa zilizopo ligi hiyo.
.
Ikumbukwe Tetesi zilidai Ronaldo kachoka na anataka kuondoka ligi iyo kurudi Ulaya akihusishwa na team kama Newcastle na Bayern munich.lakini alihojiwa na akakataa katakata tetesi izo na kusema anayo furaha kubwa kuchezea ligi hiyo ya uarabuni na hana mpango wa kuondoka.
.
Ronaldo aliongezea kwa kusema,Anawaalika nyota mbalimbali wa ulaya kuja kukipiga ligi ya Saudi kwani ni ligi yenye ushindani sana na inakua kwa kasi sana.
Kwasasa mastaa mbalimbali akiwemo Karim Benzema aliwekewa dau nono na Al itthad ya Saudi na ameshavunja mkataba na R.Madrid tayari atatua uarabuni siku za usoni kukamilisha usajili na kuanza kukipiga rasmi.Ikumbukwe Big benz alikuwa Captain na mchezaji muhimu wa R .Madrid kabla ya kuvunja mkataba by mutual agreement.
Messi,Klabu ya Al Hilal(Saudi Arabia)nayo iliweka dau nono toka mwaka jana kunasa saini ya nyota huyu wa dunia ambae ameachana na klabu yake ya PSG.Kwasasa messi anatazamia kutoa maamuzi ya mwisho huku klabu ya Inter miami(U.S.A),Klabu yake ya zamani(Barcelona) na Al hilal(Saudi arabia) zikiwa mbioni kuinasa saini ya nyota huyu.
Mastaa wengine wanaohusishwa na team za Saudi Arabia ni pamoja na Ramos (ambae nae ameachana na PSG),Alba,Busquet na Hazard ambae pia ameachana na R.madrid
Pia mwamba Ibrahim movich(Zlatan) kuna tetesi za kuhusishwa na team za uarabuni licha ya kuwa Zlatan anamiaka 42 lakini amekataa kustaafu na kuahidi kuendelea kucheza Soka,Zlatan ameachana na klabu yake ya AC millan.
Ikumbukwe pia,Kocha MuAfrika PITSO MOSIMANE amefanikiwa kuipandisha daraja klabu yake Al Ahly ya saudi Arabia kwahiyo nae atakutana na mastaa kama CR7,Benzema,Hazard n.k.
Vilevile team anayoenda Big benz ndio iliyoingiza wachezaji 9 au 10 timu ya taifa ya Saudi Arabia ambayo ndio ilivunja rekodi ya unbeaten kwa kuwachapa Argentina kwenye mechi yao ya kwanza kabisa World cup 2022.
Pia,Baadhi ya Media kubwa duniani kama ESPN,Skysports tayari wameomba vibali vya kuonesha ligi hiyo huku zikikutana na vikwazo vikali sana kwakuwa waarabu hawataki promotion za mambo ya kamari,Ulevi na upinde zinazofanywa na media hizo za ulaya.
Baadhi ya wadau wa soka wametoa maoni yao wengine wanasema wengi wanaoenda huko wanakimbia kampeni za ushoga(Upinde) kwa team za Ulaya na wengine wanadai wamefata pesa(Kula pension),
Wewe kama mdau wa soka unamaoni gani ?
Nawasilisha