Nyota kali ya Michael Jackson ilivyofifisha nyota za ndugu zake, haswa Janet na Randy ingawa Janet alikuja kuibuka tena baadaye

JOTO LA MOTO

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2018
Posts
758
Reaction score
555
Wakati wa The Jackson Five Jamii iliwapokea na kuwakubali kama kundi la Muziki lililosheheni vipaji. Baadae ilibainika kuwa Michael Jackson alikuwa na kipaji maalum kuliko wenzake, na tena haikuwa tu ni miongoni mwa kundi lao, bali ana kipaji cha kuiteka Dunia nzima. hali hii ilipelekea Jamii nayo kubaki na Michael na kuachana na ndugu zake, hatimaye kundi likaanza kupotea mdogo mdogo.

ANGALIA HAPA VITOTO JANET NA RANDY VIKIFANYA YAO.
 
Randy hakua na kipaji cha kuwafikia kaka zake hata mmoja,muondoe labda useme huyo Janet
Randy alikuwa na mvuto ingawa kipaji waweza kusema ni wastani...bado nadhani angeenda mbali kama angekaza kama sio kupotea baada ya kuachwa mbali na ndugu yao MJ.
 
Baada ya MJ nadhan Jarmaine ndio alikua anafuatia
 
Labda THE JACKSON FIVE ingeenda mbali kama sio athari za Michael.

Ilionekana kama walipoteza nguvu kwa ndugu yao kuwa Star mkubwa na Mashabiki kupoteza mvuto wa kundi.

Janet yeye alipambana aka shine kushinda wale wenzake wengine, hata wale Dada wengine, La toya na Maureen 'Rebbie' ni waimbaji lakini bado hawakufua dafu kihivyo.
 
Hapana,Baba yao ndio alikua Meneja na walikua hawaoni mafanikio yeyote kifedha alikua bado anawa treat kifamilia na watu walikua wanataka kuwekeza kwa MJ na sio kundi so kwa faida yake kimapato ilibidi aende solo
 
Exactly Mkuu...ndio nimesema hapo kuwa kundi lilipoteza mvuto baada ya Jamii yote kumtupia macho MJ.

Kwa vyovyote wasingeingiza chochote kama tayari jamii ilishapoteza mvuto nao na kubaki na MJ, including hao wawekezaji.

Nina uhakika kabisa hali ingekuwa tofauti kama Michael asingeng'aa sana na kuamua kwenda solo.
 
Exactly Mkuu...ndio nimesema hapo kuwa kundi lilipoteza mvuto bada ya Jamii yote kumtupia macho MJ.

Kwa vyovyote wasingeingiza chochote kama tayari jamii ilishapoteza mvuto nao na kubaki na MJ, including hao wawekezaji.

Nina uhakika kabisa hali ingekuwa tofauti kama Michael asingeng'aa sana na kuamua kwenda solo.
Na walichoka unyonyaji wa mshua
 
Michael Jackson alianza kuonekana jukwaani akiwa na
miaka mitano tu pamoja na kaka na dada zake.

Alitokea familia ya
wanamuziki ya Jackson Five.

Kuhusu miaka yake ya awali alisimulia mara kadhaa ya kwamba baba alimla zimisha kufanya
mazoezi mno ya kucheza na uimbaji hivyo Michael alikosa
utoto.

Watazamaji wengi wamehisi ya kwamba matatizo ya kisaikolojia ya msanii yalikuwa na chanzo katika kipindi hicho.

Michael aliandika nyimbo nyingine
maarufu ambazo ni 'Bad' na 'Black or White'.

Huyu ndiyo mfalme wa pop duniani. all the time, sijui kwanini TBC hawachezi nyimbo zake wakati alikuwa na kadi ya chama
 
Na walichoka unyonyaji wa mshua
Na inasemwa kuwa Mzee yule (Mungu amrehemu) alikuwa Dictator.

Hata MJ alilalamika kuwa Mdingi 'dictator' alichangia kumuathiri kisaikolojia kwenye ukuaji wake.
 
Michael Jackson alianza kuonekana jukwaani akiwa na
miaka mitano tu pamoja na kaka na dada zake.

Alitokea familia ya
wanamuziki ya Jackson Five.

Kuhusu miaka yake ya awali alisimulia mara kadhaa ya kwamba baba alimla zimisha kufanya
mazoezi mno ya kucheza na uimbaji hivyo Michael alikosa
utoto.

Watazamaji wengi wamehisi ya kwamba matatizo ya kisaikolojia ya msanii yalikuwa na chanzo katika kipindi hicho.

Michael aliandika nyimbo nyingine
maarufu ambazo ni 'Bad' na 'Black or White'.

Huyu ndiyo mfalme wa pop duniani. all the time, sijui kwanini TBC hawachezi nyimbo zake wakati alikuwa na kadi ya chama
Duh, kadi ya chama tena.
 
Baba yule na Mama Catherine walijaliwa uzazi, Watoto kumi na moja si mchezo.
 
FAMILIA YA JACKSON.
J FIVE.jpg
 
Back
Top Bottom