dos santos
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 256
- 128
Mchezaji nyota wa Rugby Blake Ferguson ametangaza kusilimu na kuwa muislamu katika msikiti wa zetland huko mji wa Sydney, Australia.
Ferguson mwenye umri wa miaka 23, alitamkishwa shahada ndani ya msikiti huo kama ishara ya kukubali na kuridhia uislamu kuwa ndio dini yake.
Kusilimu kwake kulihudhuriwa na waumini wengi akiwemo bondia Anthony Mundine ambaye naye amesilimu miaka mitano iliyopita karibuni.
Ferguson aliviambia vyombo vya habari kwamba ameuchagua uislamu kuwa dini yake na ana furaha kwa kuchagua uislamu.
Pia amewashukuru waliomsaidia kuutambua Uislamu na kuufuata. Ferguson ni mmoja wa wachezaji wakorofi katika ligi ya Rugby nchini Australia amepania kuwa mtu mwema kwa kupata muongozo mzuri kutoka katika Uislamu
Baada ya habari za kusilimu kwa mwanamichezo
huyo kuenea, wengi wa wanamichezo waliosilimu miaka ya karibuni walimpongeza kwa uamuzi wake wa kuwa muislamu.
source: www.ahbaabur.blogspot.com