Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu MziziMkavu mbn hujaendelea na hii kitu mkuuKwa Wale waliozaliwa huu Mwezi wa kumi Kuanzia Tarehe 24 na Mpaka kumalizikia Tarehe 21Mwezi wa kumi na moja Wasome hapa NGE – 0CT 24- NOV 21
KIPAJI CHA NG'E (MYSTICAL)
- Hii ni nyota ya 8 katika mlolongo wa nyota 12.
- Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 23 October na 21 Novemba ya mwaka wowote.
- Sayari yao ni MARS (MARIIKH).
- Siku yao ya Bahati ni Jumanne.
- Namba yao ya bahati ni 9.
- Rangi ya bahati ni Nyekundu isiyoiva au Maroon.
- Asili yao ni MAJI.
Wenye nyota hii wana kipaji na uwezo wa kiroho wa kuwasiliana na watu katika kutekeleza mambo wanayohitaji.
TABIA ZA NG'E
Wenye nyota ya Nge wana uwezo mkubwa wa uvuto au kuvutia watu katika mambo yao. Ni watu wenye uelewa mkubwa na ni majasiri katika kukabiliana na matatizo ambayo wengine yamewashinda.
Ni wenye tabia ya kutilia mkazo mambo yao, tena kwa ukali na ikibidi kutumia ukatili ili jambo litimie wao wako tayari.
Ni watu wenye tabia ya siri na wanapenda kufanya mambo yao kwa siri sana.Wenye nyota hii kama ilivyo alama yao hawaogopi kiza. Wana
uwezo na kipaji cha asili cha kutekeleza mambo yao na wakafanikiwa.
Ni watu wenye akili nyingi, waerevu na wepesi sana kuelewa mambo.
Watu wa Nge vile vile wana tabia au wanaweza kujidhuru wao wenyewe.Mambo yanapowawia magumu.
TABIA YA NG'E KATIKA MAPENZI
Watu wenye nyota ya Nge wanapenda sana kutumia fursa ya kufanya mapenzi kama njia mojawapo ya kuonyesha ujasiri wao katika mapenzi na namna wanavyojua kufanya tendo la ndoa.
Kwao mapenzi au tendo la ndoa ni kiungo muhimu sana katika maisha yao hasa ikizingatiwa kwamba nyota ya Nge inatawala sehemu za siri.Inashauriwa wale wenye moyo mdogo wasifanye mapenzi na Nge sivyo watajuta. Kitu kingine ni kwamba ni watu ambao hawayumbi na hawakubali kushindwa upesi.
Ni watu wenye ashki na hasira wakiwa wamedhalilishwa au wameumizwa na wapenzi wao na wanapofanya tendo la ndoa hasira zao huisha mara moja.
Ni watu wasiri sana katika masuala ya mapenzi na wanakuwa hivyo ili waweze kuwapata wapenzi wengi kukidhi matakwa au kiu yao kubwa ya ngono.
{mospagebreak}
TABIA YA NG'E KATIKA FEDHA
Hakuna kitu kinachoshindikana kwa wenye nyota hii, na chepesi zaidi ni namna ya kupata fedha. Wana uzoefu mkubwa wa kuhimili matatizo ya kifedha wanapoanguka, hata wakiwa matajiri na wakafilisika.
Watu wa Nge wana bahati ya kuvumbua fedha au utajiri katika njia ambazo watu wengine si rahisi kugundua.
Ni watu ambao sio rahisi kudanganyika wakiona mpango wowote wa kifedha. Mara nyingi ni kawaida yao kuchukua kitu au kufanya mradi
ambao wengine wanauona wa kipuuzi na wakaugeuza kuwa wa thamani kubwa.
Ni wakarimu sana wanapokuwa na fedha, na hawapendi kujidai kwa utajiri wao. Wako tayari wakati wowote kuwatumia watu wengine
kutekeleza malengo yao.
Kwa ujumla wao ni wataalamu wa kutafuta fedha katika njia ambazo watu wengi hawazifahamu.
MAVAZI YA NG'E
Wenye nyota ya Nge wanatakiwa wavae nguo zenye rangi inayong'ara, zenye kuonekana na maridadi,zilizo katika hali ya suti au mbili kwa pamoja.
Nguo ziwe za rangi nyekundu au shati jekundu au skafu nyekundu. Kitambaa kiwe cha sufi au cha fulana au chenye kumeremeta.
Mavazi yaendane na kofia na wanawake wapendelee sana kuvaa suruali.
MATATIZO YA KIAFYA
Nyota hii inatawala kifuko cha mkojo, uume, uke, kifandugu au kitonoko (coccy), mlango wa kizazi(cervix) na sehemu ya haja kubwa. Vile vile inatawala mfumo wa mkojo na tezi kibofu (prostate).
Matatizo yao makubwa ya kiafya yanatokana na sehemu zilizotajwa ambazo zinatawaliwa na nyota yao wenye nyota hii wanapenda kujizoesha sana mambo ya mapenzi na ngono. Wakati mwingine hisia zao zinakuwa kubwa sana kiasi kwamba wao wenyewe wanajishuku vibaya.
Inapotokea hivi wanahitajika kusafisha miili yao kwa fadhaa iliyowajaa kutokana na mfadhaiko wa hisia zao.
Kwa ujumla ni watu wenye afya nzuri na wanapona haraka maradhi yanayowasumbua. Wenye nyota hii wana tabia ya aidha kula, kunywa au kuvuta kupita kiasi au wengine hawafanyi mambo hayo kabisa.
Kwa vile nyota hii inatawala sehemu zinazoondoa uchafu wa mwili ni vizuri watu wa Nge wakawa waangalifu na mambo yanayochafua mwili wao.
Magonjwa makubwa ya wenye nyota ya Nge ni maradhi yanayohusiana na kibofu cha mkojo, maradhi ya kuziba mkojo, kansa ya tezi kibofu (prostate Cancer), matatizo ya damu ya kike na mabusha.
{mospagebreak}
KAZI ZA WENYE NYOTA YA NG'E.
Nyota ya Nge ambayo alama yake ya asili ni Maji ni nyota mojawapo ya nyota zenye nguvu katika mambo ya kikazi.
Ni watu wenye milipuko ya hisia wanapokuwa katika miradi yao ya kazi. Wanafanya shughuli zao kwa hisia kali na hamaki na wanategemea wapate majibu ya kuridhisha.
Ni watu makini sana katika kazi na wanafanya kazi kwa kutilia mkazo na ushupavu wakihakikisha wanatekeleza malengo yao. Ni watu waerevu na wenye kung'amua mambo upesi. Ni wafanyakazi wazuri na wanaheshima kwa wafanyakazi wenzao.
Kazi zinazowafaa wenye nyota hii ni kazi za madawa au tiba, kazi za upelelezi, kazi za utafiti, kazi za fundi bomba, kazi za elimu ya kale, na kazi za ushauri wa mambo ya mapenzi na ngono.
FAMILIA ZA NG'E
Wazazi wenye nyota ya Nge ni watu ambao wanaonyesha utulivu wa hali ya juu. Kimaumbile huwa hawaonyeshi hisia walizokuwa nazo juu ya watoto wao, wanaweza wakawa na chuki kubwa lakini hawapendi kuiionyesha.
Kwa ujumla wazazi hao wanapenda watoto na wanatumia muda mwingi na hisia zao kuwangalia na kuwadhibiti watoto wao.
Pamoja na ukarimu wao ni wazazi wenye kupenda nidhamu na wanataka watoto wao wafuate maadili mema. Wazazi hao walivyokuwa wadogo wamepitia ujanja wote hivyo hawakubali watoto wao wawadanganye.
Watoto watagundua kwamba wazazi wao ni watu wa kutisha na kuogopwa lakini uhusiano wao unakuwa ni mzuri. Wazazi wa kike wanakuwa na hisia kali kwa watoto wao kitendo ambacho kinawafanya watoto wawe katika shinikizo.
MADINI YA NG'E
Wenye nyota hii wanatakiwa wavae vito vinavyoitwa BERYL NA RED CORNELIUS. Mawe haya yenye rangi ya damu ya mzee (Maroon) na rangi Nyekundu yanaakisi au kuashiria asili ya Nge ya uhusiano wake wa asili na kitu chochote cha miujiza na uchawi.
UHUSIANO WA KIMAPENZI
(NG'E, NG'OMBE)
Tabia ya Nge ya wasiwasi, wivu, hisia kali za kimapenzi na dhana mbaya kwa wapenzi wao hutulizwa na kuzimwa na nyota ya Ng'ombe ambao wana tabia ya utulivu, uaminifu, wasioyumba na wanaopenda kusikiliza wanayoambiwa.
VYAKULA VYA NG'E
Wenye nyota hii wanashauriwa wale vyakula au matunda yafuatayo ambayo yanatawaliwa na nyota yao, Mananasi, wapende sana vitunguu vibichi na vilivyopikwa, Nyama ya Kondoo mchanga na vyakula viambatane na viungo vikali.
NCHI ZA NG'E
Ili kupata mafanikio ya kinyota kwa wale wenye uwezo wanashauriwa aidha kuishi au kutembelea nchi au miji ifuatayo ambayo inatawaliwa na nyota hii.
Miji hiyo ni Liverpool(Uingereza) na New Orleans(Marekani) na nchi za Poland na Switzerland.
RANGI YA NGE
Wenye nyota hii wanashauriwa wapake nyumba zao au vyumba vyao au magari yao au sehemu zao za biashara rangi nzito yenye kutia shauku na kuvutia kama rangi ya damu ya mzee (Maroon). Kila Mwezi nitakuwa nikitoa nyota moja ju ya moja Asanteni.
Mkuu MziziMkavu mbn hujaendelea na hii kitu mkuu
Haiwezekani...sijui nimtag aje akuprove wrong?!!Anza mkakati wa kutafuta mpenzi mwingine kwani huyo uliye naye anakuongopea
Na kukupotezea muda. Pole sana.
Nasubiri waliozaliwa August mkuuView attachment 1383777
NYOTA YA SAMAKI (PISCES)
Hii ni nyota ya 12 katika mlolongo wa nyota 12
Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 19 February na tarehe 20 Machi.
Sayari yao ni JUPITER (MUSHTARA)
Siku yao ya Bahati ni Alhamisi.
Namba yao ya Bahati ni 8.
Rangi yao ya Bahati ni Zambarau au Kahawia iliyochangamka.
Asili ya nyota yao ni Maji.
VIPAJI VYA SAMAKI (VISIONARY)
Wenye nyota hii wana kipaji cha kufikiria jambo na kuliunda na likawa vile walivyotaka wao.
TABIA ZA SAMAKI
Watu wenye nyota ya Samaki ni wenye huruma, wapole na wenye moyo mzuri na hawawezi kukubali kumuona binaadamu mwingine akipata taabu au uchungu. Kwa hakika ni watu ambao wana hisia kati kwa wengine ni watu ambao hawajipendelei na wako tayari wakati wowote kujitoa mhanga ili watu wanufaike, mapenzi yao au huruma kwa binadamu wengine hayana masharti yeyote.
Nafsi zao zimegawanyika katika nafsi ndogo ndogo kama vile muathiriwa mwenye kujitoa mhanga, mwokozi, na mkombozi.
Hayo yote yaliyotajwa wanaweza kuyatekeleza inapohitajiwa na ikiwa mwenye nyota hii akishatumbukia katika moja ya mambo hayo huwezi kumtoa.
Kwa ujumla nafsi za wenye nyota ya Samaki siyo za kidunia, ni watu wabunifu na wenye ndoto za kufikiri mambo ya baadaye na katika maisha yao wanaona raha sana kuwa na mawazo ambayo yatawaepusha na ugumu wa maisha.
Ikiwa wamekwama katika jambo lolote basi wataitafuta faraja au watajituliza kwa ulimwengu wao wa mawazo.
TABIA YA SAMAKI KATIKA FEDHA
Ni vigumu sana kukadiria tabia za wenye nyota hii katika fedha kwa sababau wote waliozaliwa katika nyota huwa wanachanganyikiwa kwa sababu huwa wanashindwa kutafautisha kati ya matumizi na thamani ya fedha.
Hii ni kwa sababu wanashindwa au hawakubali vikwazo kati ya muda na nafasi au za kwako na zangu, kwao kila kitu ni sawa sawa.
Pamoja na kwamba wana uroho wa pesa, uwezo na matamanio lakini wanajichukulia mambo kadri yanavyokuja. Kwao wakiwa na fedha sawa wakiwa hawana sawa vile vile kwao uwezo wa kubuni au kutunga taswira ni muhimu kuliko fedha.
Mara nyingi huwa wanajishughulisha na masuala ya kutatua matatizo ya watu wengine kuliko masuala ya kifedha. Wakati wote wako tayari kupoteza fedha kuliko kuibiwa ndoto zao.
TABIA YA SAMAKI KATIKA MAPENZI
Wenye nyota ya Samaki ni wenye kukamilika na Mahaba mengi na wanapenda sana kujitumbukiza na kuzama kwenye dimbwi la mapenzi.
Kuwa katika mapenzi ni kitu wanachokipenda na kukifurahia sana. Ni waangalifu wazuri kwa wapenzi wao wana huruma nyingi.
Ni watu wenye hisia kali za kimapenzi na ni wepesi kuathirika.
Mara nyingi huwa waoga wa vitu vya kimapenzi kwa sababu ya kuogopa kuvurugika kwa mipango yao ya baadaye.
Ni watu wenye kuyachukulia mapenzi kama ua la waridi na wanawaona wapenzi wao kama binaadamu wasio wa kawaida.
Tatizo lao kubwa la kimapenzi ni kwamba wanawaamini sana wapenzi wao na wanakuwa na mawazo au firika za kimapenzi ambazohazipo katika dunia hii.
Kwa ujumla wenye nyota hii wanapokuwa katika mapenzi wanakuwa wamejawa na shauku na mifano ya kuvutia na wanapenda wapwnzi wao waishi kiroho. Mategemeo yao yanakuwa makubwa na yaispotimia huwa wanavunjika moyo.
MAVAZI YA SAMAKI
Wenye nyota ya Samaki wanatakiwa wavae nguo za michezo kama vile fulana au za kiasili na zilizoongezwa madoido na vimbwanga vingi.
Nguo zao ziwe za rangi ya Zambarau au Kahawia iliyochangamka na rangi ya bluu.
Kitambaa kiwe cha sufu (tweed)
Wanawake wapendelee sana kuvaa sketi, ikiambatana na mikanda na viatu vyao viwe vya bati.
MATATIZO YA KIAFYA
Nyota hii inatawala nyayo na vidole vya miguu.
Matatizo yao ya kiafya yanakuja pale wanaposhindwa kutekeleza ndoto zao au mipangilio yao kimaisha au wanapokorofishana na wapenzi wao.
Wanapoathirika na hayo yaliyotajwa hukimbilia kwenye ulevi na utumiaji vidonge uliokithiri.
Tatizo lingine ni maradhi ya nyayo za miguu, uvimbe unaotokana na baridi kali hasa katika vidole vya miguu.
KAZI ZA SAMAKI
Kugunuda muelekeo wa kimaisha kwa wenye nyota hii wakati mwingine huwa ni matatizo.
Tabia yao ya kushughulikia sana binaadamu wengine huwafanya wasiwe na muelekeo.
Wenye nyota hii wanatakiwa wasifanye ubaguzi katika kazi.
Wanatakiwa wafanye kazi ambazo zinazohusiana na kusaidia watu. Kipaji cha kutafsiri mambo huwasaidia vile vile kufanya kazi za sanaa kama vile kupiga picha na kazi za muziki au maigizo.
Kazi zingine zinazowafaa ni za kuhudumia wagonjwa, kucheza shoo, uaskari wa majini (Navy) kazi za dini au kazi za kutoa ushauri nasaha (Counselling).
FAMILIA ZA SAMAKI
Wenye nyota hii ni wazazi wenye hisia, wanaopenda watoto wao na wanahuruma hasa watoto wanapowasikiliza.
Pamoja na hayo wazazi wa Samaki wana matatizo ya kukubali kwamba watoto wanaweza kuwa tofauti na wao, hata mwishowe wanapokubaliana na hilo huwa wanawachukulia watoto wao kama wageni kuliko ndugu.
Mtoto akiwa anapenda kusoma na mwenye kujituma au akiwa na tabia ya kutumia sana akili kuliko moyo huwa hapendwi na mzazi wa Samaki.
Wazazi wenye nyota hii wana mipangilio mibovu ya nidhamu na muelekeo, hivyo watoto wakorofi huwa wanatumia mwanya huo kufanya mambo yao.
Hiyo ina maana kwamba watoto wa wazazi wa Samaki wanaweza kuharibika au kutumiwa kutokana na udhaifu wa wazazi wao.
(MADINI YA SAMAKI)
Wenye nyota hii wanashauriwa wavae madini yanayoitwa.
Madini haya yanasaidia kupunguza hisia na kumuepusha mvaaji na ulevi.
UHUSIANO WA KIMAPENZI
(SAMAKI NA MASHUKE)
Tabia ya Samaki ya kuwa na mbinu na mawazo ya mambo ya baadaye huenda sambamba na tabia ya Mashuke ya utekelezaji na kujishughulisha bila kuchoka.
VYAKULA VYA SAMAKI
Wenye nyota ya Samaki wanashauriwa wapenda kula matunda au vyakula vifuatavyo.
Matunda ya Kunazi, Nyama mwitu kama Swala,nyati na kadhalika.
Vile vile wapendelee kula maboga.
NCHI ZA SAMAKI
Ili kupata mafanikio ya kinyota kwa wale wenye uwezo wanashauriwa aidha waishi au watembelee nchi au miji ifuatayo ambayo inatawaliwa na nyota yao.
Nchi hizo ni Tonga na Tanzania na miji ni Alexandria (Misri) na Seville (Ufaransa).
RANGI ZA SAMAKI
Wenye nyota ya Samaki wanatakiwa wapake nyumba zao au magari yao au sehemu zao za biashara rangi ambayo haijakoza ya Bluu au Kijani au Urujuani (violet).
Ukitaka Usafishwe Nyota yako ili ipate kung'ara na kuwa na bahati na ukitaka Pete yako ya Bahati na kinga Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr. MziziMkavu What's App +44-7459-370-172
Na mm nasubiri kwa hamu nimezaliwa agustNasubiri waliozaliwa August mkuu